Flatnews

Babu Seya Atua Mahakama ya Afrika......Awasilisha Hoja Tatu, Alia na Serikali Kuvunja Sheria

                             Hatimaye mwanamuziki, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanae, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, wametua kat...


                            
Hatimaye mwanamuziki, Nguza Viking maarufu
kama Babu Seya na mwanae, Johnson Nguza ‘Papii
Kocha’, wametua katika Mahakama ya Haki za
Binadamu Afrika (AFCPHR) Arusha.
Wanamuziki hao wamekata rufaa dhidi ya adhabu
waliyohukumiwa mwaka 2004 ya kutumikia kifungo
cha maisha gerezani.
Kupitia shauri lao lililowasilishwa mahakamani na
kupewa namba 006/ 2015, wanaiomba Mahakama
ya Afrika kutoa uamuzi kuwa haki zao zilivunjwa.
Kwa sababu hiyo wanaomba waachiwe huru na
kulipwa fidia.
Katika shauri hilo pia wameomba wawezeshwe
kupata msaada wa sheria na.
Pia wanataka Mahakama hiyo iteue wataalamu
watakaotoa ufafanuzi wa hoja za kesi yao na
kuisaidia kufikia wajibu wake.
Miongoni mwa hoja za walalamikaji hao
zilizowasilishwa mahakamani hapo ni pamoja na
kwamba mwenendo wa shauri lao haukufanyika
kwa kuzingatia haki,.
Vilevile wanadai hati ya mashtaka dhidi yao
ilikosewa kuandikwa tarehe ambayo tuhuma za
makosa yao zilidaiwa kufanywa hivyo wakashindwa
kutayarisha utetezi wao.
Pia wanadai mahakama iliyowatia hatiani
ilijielekeza katika ushahidi wa upande wa mashtaka
pekee usioshirikisha ushahidi mwingine.
Wanadai kwamba Serikali ya Tanzania kupitia
maofisa wake, ilivunja misingi ya haki za binadamu
na sheria za kimataifa.
Wanadai pia kwamba mlalamikiwa alivunja Ibara
1,2, 3, 5, 7(1)b), 13 na 18(1) ya Mkataba wa
Afrika kuhusu Ubindamu na Haki za Binadamu.
Malalamiko mingine ni kuwa baada ya kukamatwa
hawakuelezwa mapema kuhusu mashtaka
waliyokuwa wakituhumiwa nayo.
Wanadai kwa sababu hiyo waliwekwa chini ya ulinzi
kwa siku nne bila kuwa na mawasiliano na kupata
fursa ya kuonana na mwanasheria au mtu mwingine
ye yote.
Wanadai wakiwa chini ya ulinzi polisi waliwatesa
na kuwatukana na baadaye ofisa mmoja wa polisi
aliwaeleza kuwa wanatuhumiwa kwa ubakaji.
Walalamikaji hao raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo (DRC), walikuwa wakiishi na kufanya kazi
ya muziki Dar es Salaam.
Wanadai kwamba mashtaka dhidi yao yalitungwa
na hivyo hukumu iliyotolewa haikujikita katika
ushahidi wenye nguvu katika sheria.
Nguza na wanawae watatu walikamatwa Oktoba
12, mwaka 2003 na kufikishwa kituo cha Polisi cha
Magomeni Dar es Salaam.
Baadaye walipandishwa kizimbani katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu Oktoba 16 mwaka 2003.
Watuhumiwa hao pamoja na mwingine aliyejulikana
kwa jina la Mwalimu walishtakiwa kwa tuhuma 10
za ubakaji.
Pia walikabiliwa na mashtaka 11 ya kunajisi watoto
10 wenye umri wa miaka sita na nane. Watuhumiwa
wote walikana mashitaka yao.
Baada ya kusikilizwa kesi hiyo, Mahakama ya Kisutu
Dar es Salaam ilitoa hukumu Juni 25, mwaka 2004.
Iliwatia hatiani kwa kifungo cha maisha jela huku
mtuhumiwa wa tano, Mwalimu akiachiwa huru.
Walikata rufaa Mahakama ya Rufaa Tanzania
Oktoba 30 mwaka juzi ambako wafungwa wawili
Francis Nguza na Nguza Mbango walishinda rufaa
yao.
Hata hivyo, Babu Seya na Papii Kocha walijigonga
mwamba na kurudishwa jela kwa kuhukumiwa
kifungo cha maisha.
Walivyotiwa mbaroni
‘Babu Seya’ na ‘Papii Kocha’ walihukumiwa kifungo
cha maisha jela mwaka 2004 baada ya kupatikana
na hatia ya ubakaji na kuwanajisi watoto wa Shule
ya Msingi Mashujaa, Sinza Dar es Salaam.
Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa
10 ya kubaka watoto hao wa shule ya msingi
waliokuwa na umri kati ya miaka sita na minane.
Mahakama iliwatia hatiani kwa makosa mengine 11
ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huohuo kati
ya Aprili na Oktoba 2003.
Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam aliwatia
hatiani Babu Seya na wanae kwa hatia ya kubaka
na kulawiti.
Januari 27 mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia
mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu dhidi
yao.
Hukumu hiyo ilitolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu
Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Addy
Lyamuya aliyewatia hatiani kwa makosa yote
waliyokuwa wameshitakiwa nayo Juni 25, mwaka
2004.
Awali mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia
katika kesi hiyo, Babu Seya, Papii Kocha na wakili
wao, Mabere Marando walikata rufaa ya pili
ambayo ilitupiliwa mbali.
Mwaka 2010 waliomba tena rufaa ambayo marejeo
yake yalisikilizwa na kutolewa hukumu Februari
2010.
Mahakama iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha
kwa Babu Seya na Papii Kocha huku ikiwaachia
huru watoto wake wawili, Nguza Mbangu na
Francis Nguza.
Credit:Mtanzania

Post a Comment

emo-but-icon

item