IKIWA BADO SIKU 1 TU KUPIGA KURA UPEPO UMEGEUKA MGOMBEA WA CHAMA HIKI "AMFAGILIA" LOWASSA TENA HADHARANI
Mgombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia chama cha APPT– Maendeleo, Elisiana Tabwe, amewataka Watanzania wasipoteze bahati y...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/10/ikiwa-bado-siku-1-tu-kupiga-kura-upepo.html
Mgombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia chama cha APPT–
Maendeleo, Elisiana Tabwe, amewataka Watanzania wasipoteze bahati ya
kutomchagua mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
Edward Lowassa, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Tabwe alimmwagia sifa Lowassa kupitia Chadema juzi wakati wa mdahalo wa
wagombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini uliofanyika Ngokolo na
kuandaliwa na Radio Faraja mjini humo kuwa Lowassa ndiye Rais anayefaa
kuongoza nchi.
“Ndugu zangu, najua mtanishangaa, lakini bila kumung’unya maneno wala
kushinikizwa na yeyote, nawaombeni katika uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka
huu, mkamchague mgombea urais Lowassa, kiongozi ambaye mnatambua
utendaji wake wa kazi,” alisisitiza Tabwe. Hata hivyo, mgombea ubunge wa
Chadema katika Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi, na mgombea
wa CCM, Steven Masele, walikacha mdahalo huo.
CHANZO: NIPASHE
