BENZEMA AIPELEKA MADRID KILELENI LA LIGA, RONALDO AKWAMA KUVUNJA REKODI
Karim Benzema amefunga magoli mawili yaliyoipeleka Real Madrid kileleni mwa La Liga baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi y...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/09/benzema-aipeleka-madrid-kileleni-la.html
Karim
Benzema amefunga magoli mawili yaliyoipeleka Real Madrid kileleni mwa
La Liga baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Athletic
Bilbao.
Benzema sasa amefikisha jumla ya
magoli matano kwenye ligi ya Hispania msimu huu, alifunga goli la kwanza
akitumia makosa ya beki Mikel San Jose aliyekuwa akimrudishia mpira
golikipa wake.
Golikipa wa Madrid Keylor Navas
alikaribia kuvunja rekodi ya ‘clean sheet’ kwenye klabu hiyo iliyowekwa
miaka 40 iliyopita lakini Sabin Merino aliisawazishia timu yake na
kuharibu mipango hiyo.
Benzema aliifungia Real Madrid
goli la pili na kuipeleka timu yake hadi kileleni mwa msimamo wa La Liga
kufuatia kichapo walichokipata Barcelona cha goli 4-1 mbele ya Celta
Vigo.
Cristiano Ronaldo amebakiza
magoli matatu ili avunje rekodi ya kuwa mfungaji mwenye magoli mengi
ndani ya klabu hiyo inayoshikiliwa na Raul Gonzalez lakini leo ametoka
kavu.
Nyota huyo wa Ureno aliingia
uwanjani akiwa na jumla ya magoli 321 aliyoifungia Madrid kwenye
michuano yote lakini alijikuta akitoka nje ya uwanja bila kutikisa
nyavu.
