Bavicha waushambulia msimamo wa CCM kuwabana wapinzani
Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Patrobas Katambi akijadili jambo na Katibu Bavicha Taifa, Julius Mwita.
https://samchardtz.blogspot.com/2015/08/bavicha-waushambulia-msimamo-wa-ccm.html
Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, Patrobas Katambi akijadili jambo na Katibu Bavicha Taifa, Julius Mwita.
Katibu Bavicha Taifa, Julius Mwita akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
VIONGOZI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) Bavicha wamesema mwenendo unaofanywa
na serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya wapinzani si wa haki,
hivyo hawatauvumilika kamwe.
Viongozi hao ni Patrobas Katambi,
Mwenyekiti wa Bavicha Taifa na Julius Mwita Katibu Bavicha Taifa
walisema matukio mengi sana yamekuwa yakitokea dhidi ya wapinzani na
chanzo cha ni CCM, kitu ambacho wanasema kuwa hawatakivumilia kiendelee.
Wakitoa mfano, viongozi hao wamesema katika
majimbo ya uchaguzi wamejitangazia kuwa wameshinda bila kipingamizi
kitu ambacho si cha kweli.
Majimbo wanayosema kuwa wameshinda tayari
yameishakatiwa rufaa na ziko Tume ya Taifa ya Uchaguzi lakini CCM
wanaendelea kusema kuwa wameshinda bila kikwazo.
Vilevile walipinga vikali hatua ya serikali ya kuwapiga marufuku wapinzani kutumia helikopta katika kampeni zao, jambo ambalo linaonyesha wazi kuzibana siasa za upinzani.
Vilevile walipinga vikali hatua ya serikali ya kuwapiga marufuku wapinzani kutumia helikopta katika kampeni zao, jambo ambalo linaonyesha wazi kuzibana siasa za upinzani.
“Uchaguzi huu si wa CCM wala si wa Polisi
bali ni wa Watanzania wote, hivyo ni lazima haki ifuate mkondo wake kwa
kila idara iliyopewa mamlaka ya kusimamia suala fulani,” alisema Mwita.
Waliongeza kusema kuwa kama serikali haitasimamia haki wanao uwezo wa kuhamasisha vijana nchi nzima na kitakachotokea asilaumiwe mtu, alisema kiongozi huyo.
Waliongeza kusema kuwa kama serikali haitasimamia haki wanao uwezo wa kuhamasisha vijana nchi nzima na kitakachotokea asilaumiwe mtu, alisema kiongozi huyo.
