Urais UKAWA Hali Tete......Lipumba Asusa Kuhudhuria Kikao
Vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) jana vimeshindwa kumtangaza mgombea urais kama ambavyo ilikuw...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/07/urais-ukawa-hali-tetelipumba-asusa.html

Vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) jana vimeshindwa kumtangaza mgombea urais kama ambavyo ilikuwa imetangazwa hapo awali huku wakiahidi mgombea huyo kujulikana ndani ya siku ya siku saba.
Aidha, Jana kulikuwepo na kikao cha vyama vinavyounda ukawa
kilichofanyika kuanzia saa 4.00 asubuhi kwenye Hoteli ya Colosseum
jijini Dar es Salaam, lakini baadhi ya wafuasi wa Ukawa akiwemo
Mwenyekiti Profesa Ibrahim Lipumba, Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif
Hamad na naibu wake wa Bara, Magdalena Sakaya walisusia kikao hicho
suala linalozua maswali mengi kwa wafuasi wa vyama hivyo pamoja na
wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia amesema
kwamba mazungumzo yamekamilika na mgombea urais wa Ukawa atajulikana
ndani ya siku saba huku akisisitiza kuwa hakuna mpasuko ndani ya umoja
huo.
Inadaiwa kuwa hoja kubwa ilikuwa katika suala la mgombea urais,
nafasi ambayo inawaniwa na Profesa Lipumba ambaye aliyechukua fomu
kupitia CUF na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa ambaye
anakubalika na kuungwa mkono na vyama vyote vinne.
Kwa upande mwingine kutohudhuria kikao hicho kwa viongozi wa CUF
kunaweka giza nene mbele ya vyama vinavyounda Ukawa ambavyo ni
Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na NLD
Hata hivyo, kumekuwa na tetesi katika mitandao mbalimbali ya kijamii
kwamba Mbunge wa Monduli Edward Lowassa ana mpango wa kutimkia upinzani
mara baada ya jina lake kukatwa CCM, hata hivyo Lowassa hajaweza
kuzungumzia suala hilo na kuahidi kuandaa mkutano na waandishi wa
Habari kwa lengo la kutangaza mipango yake katika siasa.