TIMU YA WATU 39 KUTOKA AFRIKA KUSINI WAPNDA MLIMA KILIMANJARO KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA KUSAIDIA KUNUNUA TAULO MAALUMU KWA WASICHANA WALIOPO MASHULENI PINDI WAWAPO KATIKA HEDHI
Timu ya watu 39 wakiwasili katika lango la Marangu tayari kuanza Changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/07/timu-ya-watu-39-kutoka-afrika-kusini.html
 |
Timu
ya watu 39 wakiwasili katika lango la Marangu tayari kuanza Changamoto
ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia
kununua taulo maalumu kwa wasichana waliopo shuleni zisaidie wakati
wanapokuwa kwenye siku zao za Hedhi. |
 |
Katika
timu hiyo wamo wakurugenzi wa taasisi mbalimbali za nchini Afrika
Kusini ,watu maarufu ,watangazaji katika vituo vya Luninga,wachezaji
filamu n.k. katikati hapo ni Ofisa Uhusiano wa nje wa kampuni ya
Mawasiliano ya Vodacom nchini Afrika kusini,Maya Makanjee. |
 |
Muigizaji
maarufu wa filamu,Jack Devnarain akijulikana kama Rajesh Kumar katika
tamthiliya ya Isidindo the Need akiwasili katika lango la Marangu tayari
kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro. |
 |
Mhifadhi
mkuu Hfadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Erastus Rufunguro akizungumza
wakati akitoa historia fupi ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro. |
 |
Baadhi ya washiriki katika changamoto hiyo. |
 |
Mwanzilishi
wa taasisi ya Imbumba Foundation ,Richard Mabaso akizungumza lengo la
safari hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro ijulikanao kama Trek4 Mandela
ambayo ni mahususi kwa ajili ya kuchangisha fedha zausaidia wasichana
walioko mashuleni. |
 |
Baadhi ya washiriki katika changamoto hiyo. |
 |
Katibu
tawala wilaya ya Moshi ,Remida Ibrahim akizungumza kwa niaba ya mkuu wa
wilaya katika hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya wageni hao kabla ya
kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro. |
 |
Baadhi ya washiriki wa Changamoto hiyo. |
 |
Mkurugenzi
wa Utalii wa Shirika la Hifadhi ya taifa Mlima Kilimanjaro,Ibrahim Musa
akitangaza ofa kwa mcheza filamu maarufu wa nchini Afrika Kusini Jack
Devnarain (Rajesh ) kuja nchini kucheza sehemu ya filamu zake katika
moja ya hifadhi za Tanzania. |
 |
Mcheza
filamu maarufu nchini Afrika Kusini,Jack Devnrain(kulia) akituma picha
mbalimbali za tukio hili kwenye mitandao ya kijamii. |
 |
Mkurugenzi mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla hiyo. |
 |
Washiriki wa changamoto hiyo. |
 |
Jack Devnarain maarufu kama Rajesh Kumar wa kwenye tamthiliya ya Isidingo the Need akifuatilia matukio katika hafla hiyo. |
 |
Ofisa
Uhusiano wa nje wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom nchini Afrika
Kusini ,Maya Makanjee akifuatilia matukio katika hafla hiyo. |
 |
Ofisa
Uhusinao wa nje wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom ,Maya Makanjee
akizungumza jambo katika hafla hiyo kabla ya kuanza safari ya kupanda
Mlima Kilimanjaro. |
 |
Baadhi ya washiriki. |
 |
Washiriki wa Changamoto hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania,Allan Kijazi. |
 |
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa ,Tanzania ,Allan Kijazi akiwa na
Mkurugenzi wa Utalii wa shirika hilo,Ibrahimu Musa wakiongozwa na
Mhifadhi Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Eva Mallya
kuelkea eneo maalumu kwa ajili ya kuanzisha safari ya kupanda mlima
Kilimanjaro. |
 |
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA) Allan Kijazi
akikabidhi bendera za taifa la Tanzania na Afrika Kusini kwa kiongozi wa
timu hiyo Richard Mabaso ikiwa ni ishara ya kuanza kupanda Mlima
Kilimanjaro. |
 |
Baadhi ya wageni hao wakipia "Serfie"kabla ya kuanza kupanda Mlima. |
 |
Safari ya kupanda Mlima ndio imeanza. |
 |
Rajesh wa Isidingo the Need akiwa miongoni mwao. |
 |
Ofisa
Uhusiano wa nje waKampuni ya Mawasiliano ya Vodacom,Maya Makanjee ni
miongoni pia mwa wapandaji hao hapa akiianza safari"Pole pole"
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. |