Mwigulu achukua fomu ya Ubunge na kutoa vitisho kwa wagombea wa nafasi hiyo Iramba
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akiwa katika usafiri wa bodaboda akiingia kwenye ofisi ya CCM Wilaya ya Iramba ikiwa ni ...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/07/mwigulu-achukua-fomu-ya-ubunge-na-kutoa.html
Naibu
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akiwa katika usafiri wa bodaboda
akiingia kwenye ofisi ya CCM Wilaya ya Iramba ikiwa ni moja ya staili ya
kuwaomba kura wapiga kura wa jimbo la Iramba.
Mwigulu
Nchemba akiwasili Ofisi za chama cha Mapinduzi Wilaya ya Iramba,Mamia
ya Wananchi walijumuika naye kumsindikiza ili awezekuchukua Fomu hiyo na
hatimaye kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi kuwa Mgombea Ubunge Wilaya ya
Iramba.
Mgombea
ubunge kwa tiketi ya CCM akisaini kitabu cha mahudhurio baada ya
kuwasili katika ofisi ya CCM wilaya ya Iramba na kushoto kwake ni mke
wake mpendwa akimsindikiza kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya kiti cha
ubunge.
Naibu
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akijiandaa kumkabidhi katibu wa CCM
Wilaya ya Iramba,Bwana Mathiasi Shidagisha shilingi milioni nne kwa
ajili ya kuchukua fomu pamoja na mchango wa kuimarisha chama.
Naibu
waziri wa Fedha, Bwana Mwigulu Nchemba (wa kwanza kulia) akimkabidhi
katibu wa CCM wilaya ya Iramba, Bwana Mathiasi Shidagisha shilingi
milioni nne kwa ajili ya kuchukua fomu pamoja na mchango wa kuimarisha
chama.
Mwigulu
Nchemba akimtambulisha Mke wake Bi.Neema Mwigulu kwa Wananchi waliofika
kushuhudia Mbunge wao akichukua fomu ya kuwania Ubunge kwa mara
nyingine katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
Mke
wa Naibu waziri wa Fedha akiwasalimia wananchi waliofika kumpokea mume
wake kuchukua fomu ya kuomba kuchaguliwa tena kugombea ubunge wa jimbo
la Iramba.
Na Jumbe Ismailly,Iramba
BAADA
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupuliza kipyenga cha kuwaruhusu wanachama
wake kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi za ubunge na
udiwani,Naibu Waziri wa Fedha,Lameck Nchemba Mwigulu ameanza kutoa
vitisho kwa wagombea wengine wa nafasi hiyo.
Mwigulu
ameanza kutoa vitisho hivyo baada ya kupata habari kutoka kwa wapembe
wake kwamba kuna mgombea mmoja wa chama hicho aliyechukua fomu ya
kugombea ubunge ametangaza kuwanunua wapambe wake ili aweze kuibuka
kidedea katika kinyang’anyiro hicho.
Kwa
mujibu wa Mwigulu mgombea yeyote yule aliyeandaa pesa nyingi kwa ajili
ya kuwaanunua mawakala wake,vile vile anatakiwa kuandaa majibu juu ya
pesa hizo nyingi amezipata wapi.
“Wengine
wanasema wameandaa pesa nyingi kununua mawakala wangu,mimi niwaambie
aliyeandaa pesa nyingi kunua mawakala wangu anatakiwa pia aandae majibu
juu ya hizo pesa nyingi amezitoa wapi?”alihoji Mwigulu huku
akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Huku
akijifananisha na hayati Moringe Sokoine,Mwigulu ambaye amewahi kushika
nafasi ya Naibu katibu mkuu wa CCM Taifa,hakusita kuwatahadharisha
baadhi ya wagombea wa nafasi hiyo kwamba wasidhani watu wale waliokuwa
wakimwita Sokoine wa pili wanamtania,badala yake wajiandae kutoa maelezo
ya kule walikozipatia pesa hizo za kuwanunua mawakala wake ili aweze
kuibuka kidedea katika kinyang’anyiro hicho.
“Anadhania
wale waliokuwa wananiita Sokoine wa pili walikuwa wanatania,hivyo
anayesema ameandaa pesa nyingi atanunua mawakala wangu aandae pia majibu
kwamba hizo pesa nyingi amezitoa wapi”alisisitiza huku akiwaangalia
wananchi kwa hasira.
Aidha
Mwigulu aliyeonyesha kukerwa na kauli ya mmoja wa wagombea wa nafasi
hiyo,hata hivyo hakusita kutoa vitisho kwa wapinzani wake kwamba
unapotangaza vita huku ukiwa kwenye nyumba ya vioo unatakiwa pia
ujitathimini sana.
Huku
akijiamini kuibuka na ushindi,mgombea huyo alisisitiza pia kwamba
kutokana na kazi zilizofanyika wakati wa kipindi cha uongozi wake,hivyo
ana uhakika wa kuibuka kidedea katika mpambano huo.
“Na
taasisi zetu zinazosimamia uchaguzi zitasimamia,na taasisi zetu
zinazosimamia maadili zitasimamia,lakini baada ya uchaguzi aliyeandaa
pesa nyingi za kununua mawakala wangu aandae pia na majibu kwamba pesa
zile amezitoa wapi”.alisisitiza Mwigulu.
Hata
hivyo Naibu waziri huyo wa fedha aliweka bayana kwamba kuandaa pesa
siyo tatizo bali kuandaa majibu ya mtazania maskini anayetokea eneo
maskini ambako watu wanaokula mlo mmoja wamechanagia maabara hiyo pesa
nyingi ikiwa haipo,lakini ya kununua mawakala wote itatoka wapi,ili
watanzania waweze kufahamu inakotoka pesa hiyo isiyoweza kuchangia
maendeleo na badala yake kununua mawakala.
Akimkabidhi
fomu baada ya kulipa shilingi milioni nne,zikiwemo shilingi laki moja
za fomu na 3,900,000/= za kuchangia chama,katibu wa CCM wilaya ya Iramba
na mkurugenzi wa uchaguzi wilaya ya Iramba,Mathiasi Shidagisha alitumia
fursa hiyo kuwatahadharisha wapembe wa wagombea wote kuacha lucha za
kukashifiana.
“Kuanzia
tarehe 20 tutaanza kazi ya kuwatembeza hawa wakubwa na nimewaambia
waliokuja kuwa hatutaki kashfa wala kukashifu mwenzake…na Mh Mwigulu
najua ni Mbunge wetu lakini ubunge wako sasa hivi unaanza upya tena
ninaruhusu ufanyekazi kuanzia leo na tutawazungusha matawi yote
135”alifafanua Shidagisha.