KUMBE MANCINI ALIKUWA AKIMUONEA WIVU MOURINHO!!
Roberto Mancini amekiri kwamba alikuwa akimuonea wivu Jose Mourinho kushinda makombe matatu wakati alipokuwa akiifundisha Inter na kuon...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/07/kumbe-mancini-alikuwa-akimuonea-wivu.html
Roberto Mancini amekiri kwamba
alikuwa akimuonea wivu Jose Mourinho kushinda makombe matatu wakati
alipokuwa akiifundisha Inter na kuongeza kuwa amefanya maamuzi ya
kipuuzi kurudi kuifundisha klabu hiyo kwa mara nyingine tena.
Licha ya kushinda kombe la ligi
kuu nchini humo mara tatu mfululizo katika kipindi chake cha mwanzo,
Muitaliano huyo alifukuzwa na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho
katika msimu wa majira ya joto wa mwaka 2008.
“Sikutarajia kufukuzwa”, Mancini aliiambia Gazzetta TV.
“Nilisoma habari kutoka katika
gazeti moja asubuhi ya siku hiyo, na wasiwasi fulani hivi ukanijia.
Massimo Moratti aliniita na kuniambia kwamba yale ndio maamuzi
aliyochukua.
“Alimtaja Mourinho? Hapana. Sio
mbaya acha tu nimshukuru Moratti, kwa sabbabu alinipa fursa ya kuwa
kocha wa Inter kwenye wakati ambao ulikuwa ni muhimu sana katika maisha
yangu”.
Alipoulizwa kuhusu Mourinho,
Mancini alijibu: “Nadhani ni kocha mzuri. Je nina wivu juu ya makombe
matatu? Hizi ni fikra zilizopo ndani, lakini naamini vitu hivi vilitokea
kwa sababu vilipangwa kutokea”.