Ugaidi:Rais wa Somalia ataka ushirikiano
Rais wa Somalia Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamoud, amesema kuwa Somalia na Kenya zinafaa kuim...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/04/ugaidirais-wa-somalia-ataka-ushirikiano.html
Rais
wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamoud, amesema kuwa Somalia na Kenya
zinafaa kuimarisha
uhusiano wao dhidi ya ugaidi, baada ya wapiganaji wa
kiislamu kushambulio chuo kimoja kikuu mjini Garrisa hapo jana Alhamisi.Watu 147 waliuwawa wengi wao wakristo, baada ya wanamgambo hao wa Al- Shaabab kutumia kigezo cha kidini ili kuwatenganisha.
Bwana Mohamoud ametaja mauaji hayo kama tendo la kinyama ambalo halina msingi katika dini ya kiislamu.
Ametoa rambirambi zake kwa serikali ya Kenya.
Kenya imetoa zawadi ya shilingi millioni 5 kwa mtu yeyote atakayeweza kumkamata Mohammed Kano ,mwalimu wa zamani ambaye anashukiwa kupanga mauaji hayo.
Kwa sasa anaidaiwa kuwa nchini Somalia.