Ziara ya naibu waziri maji mkoani Njombe
Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla ametembelea mamlaka ya maji na usafi wa mazingira mkoani Njombe (NJUWASA) na kutembelea vyanz...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/ziara-ya-naibu-waziri-maji-mkoani-njombe.html
Naibu
Waziri Maji,Mh. Amos Makalla ametembelea mamlaka ya maji na usafi wa
mazingira mkoani Njombe (NJUWASA) na kutembelea vyanzo vya maji vya
Magoda,Hagafilo,Njenga na Kibena pia Amekagua ujenzi wa mradi wa
kuboresha maji mji wa Njombe kuanzia kwenye chanzo cha Mto
Njenga,ulazaji mabomba na matanki makubwa.
Mradi
wa Njenga utagharimu kiasi cha sh. 3.5 bilioni na tayari umeshagharimu
sh 2.2 bilioni na utakamilika mapema machi mwaka huu na kuongeza
upataikanaji maji kutoka asilimia 43 hadi asilimia 79,Amewataka
wakandarasi wote wa mradi huu kukamilisha kazi hiyo mapema mwezi machi
ikiwa ni kuanzia chanzo,mabomba na matanki ili wananchi mji Njombe
wapate maji ya uhakika.
Aidha amefanya mkutano na wadau wote wa maji mji wa Njombe
Naibu waziri akipata maelezo ya chanzo cha maji cha Hagafilo kutoka kwa mdau wamazingira na mlezi wa Walei ndg Edwin kilasi.
Naibu
Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akielekeza jambo wakati akipatiwa maelezo
kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji mkoa wa Njombe,Ndg. Daudi
Majani.
Naibu
Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akiangalia uunganishaji na ulazaji wa
mabomba maeneo ya airport,kambarage,nzerengerendete na Magereza.
Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akizungumza jambo na Katibu Chama cha Mapinduzi wilaya ya Njombe,Clement Mponzi.
Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akiongea na wadau maji Njombe.
Naibu Waziri Maji,Mh. Amos Makalla akikagua chanzo cha maji Magoda,Mkoani Njombe. SOMA ZAIDI