Tanzania yataja kikosi kuikabili Rwanda
Kocha wa timu ya soka ya Tanzania Mdachi Mart Nooij
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/tanzania-yataja-kikosi-kuikabili-rwanda.html
Kocha wa timu ya taifa ya soka Tanzania, Mdachi Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 26 kitakachoivaa Rwanda katika mechi ya kirafiki itakayochezwa Mwanza, ukanda wa ziwa Victoria. Kaskazini Magharibi mwa Tanzania hapo January 22.
Rwanda itakuwa mwenyeji wa fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani.
Wachezaji hao na timu zao katika mabano ni makipa Aishi Manula (Azam), Benedict Tinoco (Kagera Sugar), Peter Manyika (Simba) wakati mabeki ni Miraji Adam, Andrew Vincent (Mtibwa Sugar), Gadiel Mbaga (Azam), Emmanuel Semwanda (African Lyon) Joram Mgeveke ( Mwadui), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Edward Charles (Young Africans).
Viungo ni Salum Telela ( Yanga) , Adam Salamba (Bulyankulu FC) wakati Hassan Banda, Mohammed Hussein, Said Makapu na Said Ndemla wakiwa ni wachezaji wa Simba Sports Club.
Viungo wengine ni Hussein Malombe (Geita Gold SC), Shiza Ramadhani (Mtibwa Sugar), Omar Nyenje (Ndanda FC), Hassan Dilunga (Yanga) na Alfredy Masumbakenda ( Bulyankulu SC).
Washambuliaji ni Aboubakar Mohammed (White Bird), Kelvin Friday (Azam FC), Simon Msuva (Yanga), Atupele Mwaisemba na Rashid Mandawa (Kagera Sugar).
Timu hiyo itakuwa na kambi mbili, moja itakuwa Dar es Salaam na baadhi ya wachezaji watafanya mazoezi Mwanza. Kambi hizo zitaanza Jumapili.