MAZISHI MKE WA BILIONEA MIL. 200, WAOMBOLEZAJI WALA, WANYWA, WASAZA
Carista Charles Makoi enzi za uhai wake.
https://samchardtz.blogspot.com/2015/01/mazishi-mke-wa-bilionea-mil-200.html
MAZISHI
ya Carista Charles Makoi, 52, (pichani), ambaye alikuwa mke wa
mfanyabiashara bilionea jijini hapa, Charles Makoi yamefanyika huku
shilingi milioni 200 zikisemekana kuteketea kwa bajeti.
Mfanyabiashara
maarufu jijini hapa, Patrick Ngiloi ambaye ni mmiliki wa vituo vya
mafuta vya Kampuni ya Panone ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya
mazishi hayo.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia ajali iliyosababisha kifo cha Carista Charles Makoi.Kwa
mujibu wa chanzo makini ndani ya kamati hiyo, siku ya kwanza tu baada
ya kifo hicho, saa tatu mbele zilichangwa zaidi ya shilingi milioni 75
na baada ya hapo ziliendelea kuchangwa hadi kufikia lengo.
Chanzo
kilisema kuwa, wachangaji wakubwa walikuwa wafanyabiashara wakubwa
kutoka mikoa ya kaskazini mwa Tanzania, ikiwemo Arusha, Kilimanjaro na
Tanga.“Wengi waliowahi kuchanga ni wafanyabiashara wa mikoa hiyo
niliyokutajia. Lakini tulidhamiria bajeti iwe ya milioni mia mbili.
Unajua shughuli ni shughuli siku zote