Raia 67 wa Afrika Kusini wafariki kwa kuangukiwa na jengo la kanisa la TB Joshua
Raia 67 wa Afrika Kusini wamepoteza maisha baada ya kuangukiwa na jengo la mhubiri maarufu wa Nigeria, TB Joshua.
https://samchardtz.blogspot.com/2014/09/raia-67-wa-afrika-kusini-wafariki-kwa.html
Raia 67 wa Afrika Kusini wamepoteza maisha baada ya kuangukiwa na jengo la mhubiri maarufu wa Nigeria, TB Joshua.
Waokoaji
wanadai kuwa hostel hiyo ya kanisa ambalo huishi wafuasi wa Nigeria na
wa kigeni wa mhubiri huyo, lilianguka kutokana kuzidiwa na ujenzi wa
ghorofa zingine. Awali mhubiri huyo alidai kuwa ni watu wachache tu
walijeruhiwa na kudai kuwa ndege iliyokuwa ikipaa chini chini ndio
iliyosababisha ajali hiyo.
Jumanne alitumia Twitter kuandika; “Hard times may test me, they cannot destroy me.”
Rais
wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameagiza idara za serikali kusaidia
familia za wahanga kwenda Nigeria kutambua miili ya wapendwa wao na
kuirejesha nyumbani.