HotNews_Watatu Wakamatwa Kwa Kudurufu Kazi za Wasanii_Kigoma
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Jaffari Mohamed, akionyesha baadhi ya CD ambazo watuhumiwa walikutwa nazo.
https://samchardtz.blogspot.com/2014/09/hotnewswatatu-wakamatwa-kwa-kudurufu.html
![]() | |
| Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Jaffari Mohamed, akionyesha baadhi ya CD ambazo watuhumiwa walikutwa nazo. |
Kamanda
wa Polisi Mkoani Kigoma, Jaffari Mohamed, amesema kuwa Septemba 16
mwaka huu majira ya saa tano na nusu asubuhi katika mtaa wa Mwanga
Manispaa ya Kigoma Ujiji, askari polisi waliwakamata watu watatu ambao
walikuwa wakidurufu kazi za wasanii wa hapa nchini na nje ya nchi.
“Tumewakamata
wakiwa na Computer Laptop 5, Desktop 4 na CD 220, wako mahabusu na
tukamilisha upelelezi ili wafikishwe mahakamani,”alisema Kamanda
Jaffari.
Aliwataja
watu hao kuwa ni Alhamud Shabani mwenye umri wa miaka 19, mkazi wa
Mlole, Abeid Adam miaka 19, mkazi wa Mwanga na Ayub Huein miaka 21,
mkazi wa Mwanga Majengo Manispaa ya Kigoma Ujiji.
