Picha: Beyonce ajibu kwa vitendo tuhuma za kuhariri picha inayoonesha sehemu ya mwili wake
https://samchardtz.blogspot.com/2014/09/picha-beyonce-ajibu-kwa-vitendo-tuhuma.html
Jana
mashabiki walimshambulia Beyonce kwa picha aliyopost kwenye Tumblr
ikiwa ni moja kati ya picha za kusherehekea siku yake ya kuzaliwa
alizopiga mapema mwezi huu, ikimuonesha akishuka
ngazi akiwa ndani ya vazi la ufukweni.
“Questionable thigh gap there, Bey. #photoshop #wonkystep #beyonce,”aliuliza shabiki mmoja.
Bado swali linabaki kuwa, je, watu maarufu huamini wanakuwa na mvuto zaidi wanapokuwa wembamba kuliko walivyo na bantu figure?
Masaa machache baada ya
tuhuma hizo kuenea, Beyonce aliamua kujibu kwa vitendo kwa picha
zinazoonesha uhalisia wa mwili wake na kwamba hakuna ‘Photoshop’.


Hata hivyo, hii sio mara
ya kwanza kwa mashabiki kumtuhumu Beyonce na Jay Z kufanya photoshop ya
picha zao ili aonekane mwenye mvuto zaidi.