List ya viwanja 7 vya ndege vilivyo busy duniani!
https://samchardtz.blogspot.com/2014/09/list-ya-viwanja-7-vya-ndege-vilivyo.html
Wakati nchi kama Tanzania inapambana kujenga viwanja vya ndege ili ndege kubwa kama za Fastjet ziweze
kutua sehemu kama Musoma, Kigoma na Arusha baada ya kuweza kufanya
safari zake kwenye mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya, Dar na Mwanza, ifuatayo
ni list ya viwanja vya ndege duniani ambayo hutoka kila mwaka.
Kiwanja
kilichoshika namba moja kwa kuwa busy kuliko vyote duniani ni kiwanja
cha Atlanta Georgia Marekani wanakotoka mastaa kama rapper T.I ambacho
kwa mwaka 2013 pekee kimehudumia abiria milioni 94.4, namba mbili
inashikwa na Beijing Capital International Airport ambacho kilihudumia
abiria milioni 83.7
Kiwanja
namba 3 ni cha London Heathrow Airport kilichobakia kwenye nafasi
hiihii ya mwaka jana ambapo kimehudumia abiria milioni 72.4 huku kiwanja
cha Tokyo Japan (Haneda) kikishika namba 4, cha tano ni Chicago O’Hare
International Airport nchini Marekani na cha sita ni Los Angeles
International Airport hukohuko Marekani.
Kiwanja
cha ndege Dubai kimeshika namba 7 kutoka namba 10 mwaka uliopita ambapo
kimehudumia abiria milioni 66.4 ambapo kiwanja cha ndege cha Paris
kimeshuka nafasi moja kutoka ya 7 mwaka uliopita na kushika ya nane
mwaka huu, ya tisa imeshikwa na kiwanja cha ndege cha Dallas/Fort na
namba 10 imeshikwa na kiwanja cha Jakarta Indonesia.
Hii
ripoti imefanywa kwa kuhusisha viwanja vya ndege karibu 2000 ndani ya
nchi 160 duniani ambapo kwenye mistari ya ziada, kiwanja cha ndege cha
Hong Kong kimebaki kushika namba moja kwa kusafirisha sana mizigo
duniani ambapo mwaka jana kilisafirisha karibu tani milioni 4.2