Flatnews

UN: MH17 huenda ni Uhalifu wa Kivita


Kutunguliwa kwa MH17 huenda ni Uhalifu wa Kivita
Afisa wa umoja wa mataifa anayesimamia haki za kibinaadamu Navi Pilay amesema kuwa kutunguliwa kwa ndege ya kampuni ya Malaysia Airline MH17 mashariki mwa Ukraine huenda ukawa uhalifu wa kivita.
Ukraine pamoja na mataifa ya Magharibi wanaamini kuwa wapiganaji wanaoungwa mkono na Urusi waliiangusha ndege hiyo kwa kutumia makombora yanayotoka Urusi.
Watu wote 290 walikuwa ndani ya ndege hiyo walifariki.
Hatahivyo waasi hao wamekana kuitungua ndege hiyo.
Afisa huyo mwandamizi wa Umoja wa Mataifa ametaka uchunguzi ulio huru kufanywa kuhusu kuangushwa kwa ndege ya Mh17.
Ameapa kwamba juhudi zote zitatekelezwa kuhakikish kuwa mtu yeyote ambaye amekiuka sheria ya kimataifa anashtakiwa.
Taarifa hiyo ya umoja wa mataifa inasema kuwa mgogoro huo umasababisha mauaji ya watu 1,100 huku serikali na waasi hao wakitumia silaha kali katika maeneo yalio na makaazi ya watu.
UN: MH17 huenda ni Uhalifu wa Kivita
Wakati huohuo majeshi ya Serikali ya Ukraine ilipata mafanikio makubwa usiku kucha dhidi ya waasi karibu na mji muhimu wa mashariki mwa Donetsk.
Bi Pillay katika ripoti yake inayohusiana na Ukraine alisema kuwa watu 1,129 wameuawa katika vita hivyo huku 3,442 wakijeruhiwa kutokana na vita hivyo vilivyozuka katikati ya mwezi wa Aprilil.
Wakti huohuo ,msemaji wa wizara ya Usalama wa Ukraine Andriy Lysenko amewaambia waandishi wa habari mjini Kiev kuwa ndege hiyo ya Malaysia MH17 ilianguka baada ya kukumbwa na mlipuko mkubwa ambao ulisababisha vilipuzi kutoboa ndege hiyo.
Msemaji huyo aliongezea kuwa visanduku viwili ya kunasa sauti vya ndege hiyo vinaendelea kupigwa msasa na wataalumu kutoka Uingereza.
Wananchi wakitoroka vita Mashariki mwa Ukraine
Kwa Upande wao Urusi wanasema kuwa wanatarajia walinda usalama wa umoja wa Ulaya OSCE watatumwa katika mpaka wa nchi hiyo na Ukraine ilikulinda amani.
Waziri wa kigeni wa Urusi Sergei Lavrov alisema kuwa japo majeshi ya serikali yameingia katika miji ya Shakhtarsk na Torez kunahaja ya kuwepo kwa wachunguzi wa kimataifa baina ya Ukraine na Urusi.
Majeshi ya Ukraine yanasema yanalenga kudhibiti miji ya Pervomaysk na Snizhne yote iliyoko karibu na eneo kulikotunguliwa ndege hiyo ya MH17.

Post a Comment

emo-but-icon

item