Flatnews

RODGERS: UKALI WA LIVERPOOL HAUJAATHIRIKA NA KUONDOKA KWA LUIS SUAREZ



BRENDAN Rodgers amepotezea majadiliano kuwa Liverpool itakuwa kwenye wakati mgumu baada ya Luis Suarez kutimkia Barcelona.
Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao 31 katika mabao 101 ya klabu hiyo msimu uliopita alijiunga na miamba hiyo ya La Liga kwa dau la paundi milioni 75 majira ya kiangazi mwaka huu.
Raheem Sterling alifunga bao pekee siku ya jumapili ambapo Liverpool iliifunga bao 1-0 Oliompiacos ikimalizia kazi nzuri ya Daniel Sturridige, wakati huo mshambuliaji mpya Lazar Markovic alionesha kiwango kizuri katika mchezo wake wa kwanza.
“Nawaona wachezaji ambao walifunga mabao 70 msimu uliopita. Ni rahisi sana,” Rodgers aliwaambia waandishi wa habari.
“Luis Suarez sio mchezaji wa Liverpool, kwahiyo sitaki kuzungumzia au kumrejea Luis Suarez”.
“Nitakuwa na wasiwasi na wachezaji nilionao, walioonesha kiwango kizuri msimu uliopita, hata tulipomkosa Luis, tuliweza kufunga magoli. Haitakuwa tatizo”.
Rodgers alisema Sturridige, aliyefunga mabao 21 kwenye mechi za ligi kuu msimu wa 2013-14, ataweza kufanya kazi nzuri tena, wakati huo aliwasifu Sterling na Markovic.
“Nimeona mabadiliko kwa Daniel tangu aliporudi,” alisema. “Kiukweli amejiamini  kutokea kombe la dunia na msimu uliopita”.
“Nadhani yupo tayari kubeba majukumu. Alifunga mabao 21 msimu uliopita, nadhani ni mshambuliaji wa thamani kubwa”.
“Markovic ataendelea kuwa bora na bora. Alionesha uimara na tunaamini atakuwa mzuri zaidi atakapopata kasi na uharaka kwenye mchezo wake, ataendelea vizuri na anakuja kumaliza”.

“Tumepata kasi nzuri. Raheen wakati wote ni hatari-anafurahisha kumtazama. Nadhani watatu hawa walifurahisha”.

Post a Comment

emo-but-icon

item