UKATILI DHIDI YA MTOTO UTAISHA LINI? AUAWA KWA KUFUNGWA PLASTA MDOMONI
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/ukatili-dhidi-ya-mtoto-utaisha-lini.html
Mtoto aliyekutwa amefariki baada ya kutupwa eneo la Kawe-Beach na kufungwa plasta mdomoni na puani.
KATIKA
hali isiyo ya kawaida mwanamke mmoja ambaye hakujulikana jina lake wala
kujua anapoishi, anasadikika kutenda ukatili na unyama wa hali juu kwa
kumuua mwanaye na kisha kumtupa pembezoni mwa barabara ya kwenda
Kawe-Beach.Wavuvi
wa eneo hilo waliona mfuko pembezoni ukiwa na damu hali ambayo
iliwashtua na kuamua kusogea karibu ndipo walipomkuta mtoto huyo mwenye
jinsi ya kike akiwa amefariki huku akiwa amefungwa plasta mdomoni na
puani.
Wakazi wa eneo la Kawe na wapita njia wakiangalia kichanga hicho baada ya kuokotwa na wavuvi.