Flatnews

Ebola yawa tishio Liberia


Nchi ya Liberia imefunga mipaka yake iliyo mingi ya kuingia nchini humo ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi mapya ya ugonjwa Ebola.
Hata hivyo katika kuongeza jitihada Zaidi nchi hiyo vituo vya uchunguzi vimewekwa katika baadhi ya mipaka ya kuingia nchini humo vikiwemo viwanja vya ndege.
Katika hatua nyingine moja ya shirikakubwa la ndege Nigeria la Arik Air limesitisha ndege zake kuelekea Liberia na Sierra Leone baada ya mtu mmoja kubaini kuwa na ugonjwa huo wakati akisafiri kwa ndege kuelekea Nigeria.
Hadi sasa virusi vya Ebola vimesababisha vifo kwa watu 660 Afrika Magharibi tangu ugonjwa huo ulipozuka mwezi February mwaka huu.
Nigeria pia inachukua tahadhali katika mipaka yake baada ya kuthibitisha kufariki kwa raia mmoja wa Liberia wakati akiwasili uwanja wa ndege wa Lagos.

Post a Comment

emo-but-icon

item