TAZAMA WAUMINI KANISA LA MORAVIAN WAZUA TIMBWILI
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/tazama-waumini-kanisa-la-moravian-wazua.html
WAUMINI wa Kanisa la Moravian lililopo
Kinondoni-Msisiri jijini Dar, jana jioni walifanyiana timbwili na wenzao
waliojitenga kwenye kanisa hilo kitendo kilichopelekea askari polisi
kuingilia kati na kutuliza ghasia hizo.
Baada ya vurugu za jana, leo asubuhi
waumini hao wameendelea kufanyiana ubabe hali iliyowalazimu polisi
kufika tena kanisani hapo na kuwasomba watuhumiwa wote na kuwapeleka
Kituo cha Polisi Oysterbay, Dar kwa mahojiano zaidi.
(PICHA/HABARI: RICHARD BUKOS / GPL)