MAMA WA VAN GAAL AANIKA SIRI ZA `BIG BOSI` HUYO WA OLD TRAFFORD!
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/mama-wa-van-gaal-aanika-siri-za-big.html
Timu ya ushindi: Louis van Gaal na Truus wamejiunga na Manchester United kuanza ukurasa mpya wa maisha ya mpira.
LOUIS
van Gaal haogopi kukosolewa na mashabiki pamoja na vyombo vya habari,
anasema mtu anayemfahamu vizuri mno kocha huyo mpya wa Manchester
United.
Mke
wake Van Gaal, Truus van Gaal, ameweka wazi kuwa kocha huyo wa zamani
wa Ajax, Barcelona na Bayern Munich, hawezi, hajawahi kukata tamaa pale
anapokosolewa isipokuwa anaumia sana anaposhindwa kufanya kazi yake
vizuri au anapomuumiza yeye.
Watu
wote wa Old Trafford watakuwa na furaha kusikia kuwa inachukua muda
mrefu kumuudhi kocha huyo mwenye miaka 62-isipokuwa mke wake
anayechukizwa na watu wanamuudhi mume wake.
Busu la kheri: Louis akimsalimia mke wake kwa kumpiga busu mke wake katika siku ya nne ya mazoezi ya kabla ya kombe la dunia.
Truus alisema: 'Louis haogopi kukosolewa"
"Hata
kama timu yake imecheza vizuri au vibaya, hata kama watu au vyombo vya
habari vitamponda au hapana, haathiriwi na kitu chochote.
"Mara zote ananiambia: "Unaogopa nini? waache wafurahie haki yao. Wewe tu ndio nakuogopa na najua mambo yalivyo kiuhalisia".
"Kitu pekee kinachomuudhi ni kuona mimi naumia au nakata tamaa".
Truus alikiri kuwa hafanani na mume wake kwasababu yeye anaguswa sana na matusi.
"Siku za nyuma, nilienda kwenye mechi ya mpira wa miguu na kulikuwa na mtu mbele yangu akamtukana Van Gaal".
"Nilimshika mabegani na kumkalipia: "Amekufanyia nini" unamjua?" mtu huyo aliogopa sana.
Kocha mpya wa Manchester United, Van Gaal, falsafa yake ni kucheza mpira wa kushambulia.