Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ukiwemo mtandao wa tracetv unaripoti
kwamba mchumba wa Shakira, Gerard Pique amekaririwa akisema hitmaker wa
‘Hips Dont Lie’ ni mjamzito kwa mara nyingine tena.
Kulikuwepo na tetesi nyingi hasa baada ya Shakira kutumbuiza kwenye
kombe la dunia liloisha hivi karibuni nchini Brazil, lakini kambi ya
Shakira ilikanusha uvumi huo.
Lakini jana kupitia channel ya kilatino ya “Fox News” – kituo hicho cha TV kiliripoti kwamba Pique amewathibishia kwamba Shakira ni mjamzito.
Pique na Shakira tayari wana mtoto mmoja wa kiume waliyempa jina la
Milan, ambaye alizaliwa mnamo mwaka 2012, miaka miwili baada ya wazazi
wake kuanza mahusiano yao wakati wa utengenezwaji wa wimbo wa kombe la
dunia 2010.