Flatnews

RASMI ORIGI ASAINI LIVERPOOL


Liverpool wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi kutoka Lille kwa pauni milioni 10. Origi, 19, amesaini mkataba wa miaka mitano, lakini atasalia Ufaransa na klabu yake ya Lille kwa mkopo kwa msimu ujao na atakwenda Anfield msimu wa 2015. Origi alicheza mechi zote za
Ubelgiji katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 na alifunga bao pekee katika mchezo dhidi ya Urusi. Alianza kucheza soka katika klabu ya Genk kabla ya kuhamia Lille akiwa na miaka 15. Origi anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Liverpool, baada ya kumchukua Rickie Lambert, Adam Lallana na Dejan Lovren kutoka Southampton, pamoja na Emre Can kutoka Bayer Leverkusen na Lazar Markovic kutoka Benfica.

Post a Comment

emo-but-icon

item