Flatnews

Manusura waanza kutoa Ushahidi Korea K


Wahudmu walituhimiza tutuliea licha ya kuwa ferry ilikuwa inazama
Wanafunzi walionusurika katika mkasa wa feri iliyozama nchini Korea Kusini mwezi Aprili wamesema kuwa waliagizwa kusalia katika vyumba vyao wakati meli hiyo ilipozama .
Walikuwa wanatoa ushahidi katika kesi inayomkabili nahodha na wafanyikazi wa meli hiyo wanaokabiliwa na mashtaka ya uzembe na mauaji kufuatia kufa maji kwa takriban watu 300 katika mkasa huo.
Mwanafunzi mmoja amesema kwamba yeye na wenzake walifuata maagizo hayo hadi pale mlango wa chumba chao ulipokuwa juu ya vichwa vyao huku maji yakiingia ndani ya feri hiyo kupitia madirishani.
Mwengine alitaka kujua ni kwa nini waokoaji hawakuingia ndani ya chombo hicho ili kuwasaidia kutoka.
Wanafunzi walikaribia kwenye milango ya kutoka ambapo walisaidiwa kutoka na wanafunzi wenzao.
Feri hii ilizama tarehe kumi na sita mwezi wa Aprili kwenye kisiwa cha Jeju ambapo watu mia tatu na wanne waliaga dunia.
Wanafunzi hao walikuwa wakitoa ushahidi katika kesi wanohukumiwa wafanyikazi wa feri hiyo.
Tulikuwa tumengoja hadi wakati ambapo maji yalianza kuingia kwenye feri ,msimamizi wa darasa alituagiza kuvaa vazi maalum la kuokoa maisha.mwanahabari wa Reuters aliiga maneno ya mwanafunzi .
Wanafunzi wananza kutoa ushahidi Korea
''Kupitia mlango uliokuwa juu yetu tuliweza kuelea na hatimaye tukatoka.wanafunzi waliotoka mbele yetu walituvuta nje ya meli hiyo.''
Wengi wa Walioaga dunia kwenye meli hiyo ya Sowel walikuwa wanafunzi kutoka shule moja ya upili waliokuwa kwenye ziara ya shule.
Wafanyikazi wanashtumiwa kwa kosa la kutomakinika na kutelekeza majukumu yao .
Nahodha na maafisa watatu pia wanakabiliwa na kosa la mauaji kwa njia ya uzembe kwa makusudi.
Wachunguzi wanasema kwamba feri hiyo ilikuwa imeundwa kinyume na sheria ili iweze kubeba abiria na mizigo zaidi,hivyo basi ilikuwa imepitisha kiwango kinachostahili.
Hata hivyo waendeshaji mashtaka walisema kuwa tendo la nahodha na wafanyikazi kuwaagiza abiria kutulia humo ndani feri hiyo ilipokuwa ikizama kulisababisha vifo zaidi.
Jumatatu ilikuwa siku ya kwanza wanafunzi hao walikuwa wanatoa ushahidi .
Baadhi ya wanafunzi walionusurika
Mwanafunzi mwingine alieleza kutoweka kwake kwa kuruka kwenye bahari.
Msichana mmoja alisema kuwa Kulikuwa na wanafunzi wengi katika ukanda wa meli ambao walizuiliwa kwenye feri hiyo.
Mkasa huu ulisababisha hasira nchini Korea Kusini ikiwemo ukosoaji mkali kwa wafanyikazi wa serikali na wanabiashara ambao wanasemekana kutowajibika katika kazi yao ama pia yawezekana ufisadi ulipelekea mkasa huo.
Mwaanzoni mwa mwezi huu,polisi walitambua maiti ya mwenye kampuni inayomilika meli hiyo Yoo Byungeun .
Mwanawe wa kiume Yoo Dae-Kyun alikamatwa ijumaa.

Post a Comment

emo-but-icon

item