Kamishina
wa polisi kanda maalum ya Daresalaam Suleimani Kova akitoa ufafanuzi
jambo kwenye mkutano na waandishi wa Habari Jijin Dar es Salaam,
JESHI
la Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam limefichua Siri ya kuongezeka
Vitendo vya ujambazi katika maBenki mbalimbali hapa nchini na kusema
vitendo hivyo vinasababishwa na Wamiliki wa Mabenki hayo kulipuuza Jeshi
la polisi,Kauli
hiyo ya Jeshi la polisi Kanda ya Dar es Salaam imekuja SIKU moja
kupita baada ya watu wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi kuvamia katika
Benki ya Stanbic tawi la Kariakoo liloko mtaa wa Swahili na kukomba
mamilioni ya pesa aliyokuwa nayo Mteja,
Kauli
hiyo imetolewa Mda huu na Kamishna wa Polisi kanda Maalum Dar Es
Salaam,Suleiman Kova wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari Jijini Dar
Es Salaam,ambapo alisema watu wanaochangia Vitendo hivyo vya Ujambazi
kuzidi kuongezeka katika Mabenki mbalimbali hapa nchini ni Wamiliki wa
Mabenki kupuuza ushauri wa Jeshi la Polisi ,
Uliowataka waache kutumia walinzi wa Makampuni Binafsi peke yake,watumia na Walinzi kutoka Jeshi la polisi.
“Nataka
niwambie waandishi hivi vitendo vya Uvamizi kwenye mabenki viemtokana
na wamiliki wamabenki hayo kupuuza ushauri wetu uliowataka kwenyes
shuhuri za Ulinzi kwenye mabenki watumike Polisi tu,lakini wao
wakapuuza,ukitaka kuamini Nenda kwenye Mabenki yanayolindwa na Polisi
kama utaona kama kunauvamini wowote uonotokea,kwasababu majambazi hao
wanashindwa kuvamia kutokana na umakini wa Jeshi la Polisi”alisema Kova
Kamishna
Kova,alisema kwa sasa Jeshi la polisi limejipanga kuongea na Benki
kuu(BOT) ambaye ni kiongozi wa Benki zote hapa nchini na kutafuta
ufumbuzi wa hili tatizo la Mabenki Mengine kupuuza ushauri huo wa Jeshi
la polisi.
Vilevile
jeshi hilo la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Limeeanza msako
kali wa kuwatafuta Majambazi watano waliovamia Jana kwenye Beki ya
Stabinc Tawi la Kariakoo lilioko mtaa wa Shwahili majira ya mchana.
Kwa
Mujibu wa Kamishna Kova alisema watu wa tatu kati yao waliingia ndani
ya Benki hiyo wakiwa na Mifuko Mikubwa wakijifanya ni wateja wanapeleka
Fedha nyingi katika Benki hiyo,watu hao walipoingia ndani walianza
kuwalazimisha kuvuka wigo wa wateja wa kwaida na kutaka kuingia kwa
nguvu kupora Fedha.
Ambapo
Benki hiyo ya Stabinc ina mitambo ya Aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na
Vingora vya Tahadhari,ikasaidia kwa majambazi hao kushindwa kuingia
ndani kuiba pesa za Benki hiyo kutokana na Vingora hivyo kupiga kelele
na kuanza kuwapa uwoga majambazi hao ,ambapo walifanikiwa kuiba pesa za
mteja mmoja ambae alikuwa anataka kuweka pesa kwenye benki hiyo,
Kova
alisema Majambazi hao walipotoka nje ya Benki hiyo walipiga Risasi Juu
ili kuwapa Hofu wananchi walikuwa Nje ya Benki hiyo,ambapo kwa Mujibu wa
Kamishna Kova anasema bado wanaendelea kuwafuatilia majambazi hao.
Katika
Hatua nyingine Jeshi hilo la polisi Limejipanga ipasavyo kwenye sikuku
ya IDD El Haji 2014,ambapo jehi hilo limesema limepanga kushikirikiana
na Vyombo mbalimbali vya ulinzi na Usalama ikiwa ni pamoja na
Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji,Kampuni Binafsi za ulinzi lengo ni
kuhakikisha wananchi wanafurahia kwa utulivu na amani kwenye sikuku hii.
|