KAKA: SIKUCHEMSHA MUDA NILIOCHEZA REAL MADRID
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/kaka-sikuchemsha-muda-niliocheza-real.html
KAKA amesisitiza kuwa kamwe hajutii maamuzi yake
ya kujiunga na Real Madrid na anahisi muda aliokaa klabuni hapo ulikuwa wa
mafanikio.
Kiungo huyo mshambuliaji alijiunga na Real Madrid
akitokea AC Milan kwa ada inayoaminika kuwa Euro milioni 65, lakini hakufikia matarajio
makubwa kwa miamba hiyo ya La Liga.
Kaka alitumia muda wake mwingi Santiago Bernabeu
kwa kukaa benchi, lakini bado anasema aliridhishwa na muda aliokaa Madrid na
kuitetea rekodi yake ya Hispania.
“Muda niliokaa Madrid sikushindwa,” Kaka
aliwaambia Globo Esporte. “Nilicheza
mechi 120, nilifunga mabao 28 na nilicheza michezo kwa wastani wa 30 kwa msimu”.
“Kipi zaidi, nilishinda makombe matatu: La Liga,
Copa del Rey na Supercopa de Espana”.
Nyota huyo mwenye miaka 32 ambaye kwa sasa
anacheza klabu yake mama ya Sao Paulo kwa mkopo, aliendelea kwa kumzungumzia
kocha wake wa zamani wa Real Madrid, Jose Mourinho kuwa alimsaidia kuimarika.
“Mourinho alinisaidia kukua. Alinifundisha kuwa
mvumilivu, kuendelea kupambana na kuheshimu maamuzi ya kocha. Alinisaidia
kuimarika na kuwa mwanaume”.
“Nilijifunza kumheshimu kocha na kujitahidi kuonesha juhudi kadiri niwezavyo nikiamini kuwa ninaweza kuwa mmoja ya watu watakaocheza. Na ndivyo nilifanya katika miaka yangu mitatu chini ya Mourinho”.