Israel kusitisha vita kwa saa 24 zaidi
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/israel-kusitisha-vita-kwa-saa-24-zaidi.html
Serikali ya Israel imekubali
kusitisha vita katika eneo la Gaza kwa sababu za kibinaadamu lakini
kundi la Hamas limesema kuwa halitakubali tena makubaliano mengine.
Afisa mwandamizi nchini Israel amesema kuwa
makubaliano hayo ya kusitisha vita yatafanyika kwa saa 24 kufuatia ombi
la Umoja wa mataifa.Msemaji wa Hamas ameiambia BBC kwamba uharibifu unao-onekana katika eneo la Gaza wakati wa mchana ndio uliowashinikiza kuendelea na mashambulizi hayo.
Ameishtumu Israel kwa kutumia makubaliano hayo kutekeleza mashambulizi zaidi.
Takriban raia 1000 wa Palestina wameuawa huku zaidi ya raia 40 wa israel wengi wao wakiwa wanajeshi wakifariki.