Flatnews

BEKI YA MANCHESTER UNITED YATIKISWA BAADA YA RAFAEL KUUMIA NA KUTIMKA MAREKANI


Manchester United's defensive worries grow as Rafael leaves US tour
BEKI wa Manchester United, Rafael, atakosa mechi zilizosalia za klabu hiyo katika ziara ya maandalizi ya kabla ya msimu nchini Marekani baada ya kupata majeruhi ya nyonga.
Beki huyo wa pembeni wa Brazil mwenye miaka 24 alipata majeruhi hayo katika ushindi wa Man United wa mabao 3-2 dhidi ya Roma siku ya jumamosi.
Ingawa ukubwa wa tatizo haujulikani, lakini taarifa hizo ni mbaya kwa kocha Louis Van Gaal ambaye anatarajia kutumia zaidi mabeki wa pembeni kupandisha mashambulizi msimu ujao.
Mholanzi huyo amewapoteza Rio Ferdinand, Nemanja Vidic na Patrice Evra waliotimka Old Trafford, na hii itampa wakati mgumu katika mfumo wake wa 3-4-1-2 ambao anawatumia mabeki watatu katikati.
Rafael alitarajiwa kucheza beki ya kulia ambayo Antonia Valencia ilikuwa anatumika kutokana na kukosa beki mwingine wa kulia.
Phil Jones na Chris Smalling walitumika kuziba nafasi ya Mbrazil huyo msimu uliopita, lakini kwasasa ndio mabeki watatu pekee wa kati wenye uzoefu waliosalia klabuni.
Rafael atakuwa anapata matibabu kwenye kambi ya klabu hiyo mjini Manchester na anatarajia kuungana na wenzake baadaye majira haya ya kiangazi.

“Rafael amerudi Manchester kuendelea na matibabu kufuatia majeruhi ya nyonga aliyoyapa wakati za mazoezi uwanja wa Denver”. Ilisema taarifa ya United iliyochapishwa kwenye mtandao wake rasmi.

Post a Comment

emo-but-icon

item