Alichojibu Ronaldo baada ya kuripotiwa kusainiwa na Lil Wayne
https://samchardtz.blogspot.com/2014/07/alichojibu-ronaldo-baada-ya-kuripotiwa.html
Baada
ya Jay Z kufungua kampuni ya kusimamia wanamichezo na kuanza kupata
mafanikio kupitia biashara hiyo, mwanamuziki mwingine nguli wa hip hop
kutoka nchini Marekani, Lil Wayne ameripotiwa kufungua kampuni ya
usimamizi wa
wanamichezo na Cristiano Ronaldo, ametajwa kuwa mchezaji wa kwanza kusainiwa na kampuni hiyo ya Wayne.
Taarifa zilizotoka mwanzoni mwa wiki hii zilisema Lil Wayne kupitia
kampuni yake atakuwa akishughulikia masuala yote ya kibiashara ya
Ronaldo ndani ya Marekani, kwa mujibu wa TMZ.
Kampuni hiyo ya Weezy’ inatajwa kuwa ingefanya kazi na kampuni ya
PolarisSports, kampuni dada na CAA na GestiFute, taasisi ambayo wakala
wa Ronaldo – Jorge Mendes ndio anaiendesha.
Lakini jana kupitia mtandao wa Twitter, Ronaldo alikanusha taarifa hizo
za kuingia kwenye ushirikiano wa kibiashara na kampuni ya Wayne, huku
akisisitiza timu yake ni ile ile na hajabadilisha chochote.
Ronaldo yupo chini ya kampuni ya usimamizi wa wachezaji ya GestiFute, ambayo pia inamwakilisha Jose Mourinho, Pepe, James Rodriguez, Moutinho, Falcao, Nani na wachezaji wengine wengi wa Ureno na Amerika ya kusini.