Watu watatu wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika ajali ya magari mawili
Na Abdulaziz Lindi
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/watu-watatu-wapoteza-maisha-na-wengine.html
Watu
watatu wamefariki Dunia baada ya Magari mawili yenye tela kila moja
kuacha njia na kupinduka na kufasabisha vifo vya watu hao na kujeruhi
wengine wawili katika ajali iliyotokea Jana Huko Tarafa ya Rondo wilaya
ya Lindi Mkoani Lindi.
Ajali
hiyo Iliyohusisha gari aina ya HOWO lenye Usajili T270BZU na Tela na
T260AZU Pamoja na Lori aina HOWO T871 BTH Tela T 626 BTT yote yaliacha
njia
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Lindi kamishna msaidizi Renatha Mzinga amethibitsha
kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja marehemu hao ambao ni Marehemu
Jackson Francis Kayombo (DEREVA) mwenye umri wa miaka 42,marehemu Lazaro
Michael Chaula,(Mkinga) miaka 27 Dereva na Marehemu Mohamed Jumanne
Said (Mmakonde) miaka 23.
Kamanda
Mzinga amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni ambao ni Given Mussa
Mohamed na Seleman Ibrahim Hamis ambapo pia alibainisha kuwa Maiti na
majeruhi wote wamefikishwa katika Hospital ya Sokoine Manispaa ya Lindi.
Aidha
kamanda Mzinga pia alieleza matukio ya mwishoni mwa wiki ambapo Wakazi
wanne wa wilaya za Nachingwea,Ruangwa na Manispaa ya Lindi, wamefariki
dunia katika matukio tafauti,likiwemo mtu anayesadikiwa kuwa na matatizo
ya akili kuwapiga vikongwe wawili mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani
hapa.
Kwa
mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani hapa,Regina Mzinga,vifo hivyo
vimetokea mei 27 na 31 mwaka huu,katika wilaya tatu kati ya tano
zilizopo mkoani hapa.
Amewataja
marehemu hao kuwa ni,Mwanahawa Said (65) na Bakari Maurusi (70) wakazi
wa kijiji cha Mpiruka,wilaya ya Nachingwea,Mahamudu Issa wa kijiji cha
Mbagala,wilaya ya Ruangwa na Hadija Seifu (10) mkazi wa mtaa wa kariakoo
Manispaa ya Lindi.
Mzinga
amefafanua kwa kueleza kwamba,Mwanahawa na Maurusi wamepoteza maisha yao
mei 27 mwaka huu,mchana baada ya kupigwa kwa rungu kichwani na mtu
aitwae Agnes Mathayo,anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili,wakati ndugu
zao wakiwa mashambani.
"Hawa
vikongwe wawili na huyu muuwaji Agnes walibaki nyumbani,wakati jamaa zao
wengine walikwenda kushughulikia mazao mashambani mwao"Alisema Mzinga.
Kamanda
huyo wa Polisi mkoani Lindi,amesema tayari mtuhumiwa Agnes Mathayo
ameshakamatwa na kushikiliwa kituo cha wilaya kilichopo mjini
Nachingwea, akisubiri kufanyika kwa utaratibu wa kumpeleka Hospitali ya
kupima akili kabla ya kumfikisha Mahakamani.
Akasema
Mahamudu Issa,ambaye alikuwa ni mwalimu mstaafu amefariki mei
27/2014,saa 1:30 baada ya kuamua kujinyonga kwa kujitundika juu ya mti
aina ya mkorosho uliokuwepo karibu na nyumba yake kwa madai ya ugumu wa
maisha,kutokana na kuishiwa fedha za malipo ya kustaafu
Katika
tukio la tatu,kamanda Mzinga akasema mtoto Hadija Seifu amepoteza uhai
wake mei 31 mwaka huu,saa 3:05 asubuhi,baada ya kugongwa na gari ndogo
aina ya Hiace katika barabara kuu itokayo mjini Lindi kwenda mikoa ya
Mtwara na Ruvuma.
Ameeleza
kuwa Hiace hiyo yenye namba za usajili T. 354 CRM ilikuwa ikiendeshwa na
Abdull Mohamedi (32) mkazi wa mtaa wa kariakoo Manispaa ya Lindi,na
kwamba dereva huyo atafikishwa Mahakamani muda wowote baada ya
kukamilika kwa taratibu za kisheria