Picha Maalum Kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa:Tazama Picha Mbalimbali Za Ushiriki wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe Katika Sherehe za Kumuapisha Mkuu wa Majeshi wa Zamani, Field Marshal Abdel Fattah al Sisi kuwa Rais mpya wa Misri
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/picha-maalum-kutoka-wizara-ya-mambo-ya.html
Sehemu
ya mto Nile ambapo kando yake ndiyo kuna Hoteli ambayo Waheshimiwa
Mawaziri waliandaliwa chakula cha jioni. Angani ni helikopta ikiwa
katika doria kuhakikisha kuwa hakuna mtu anadhurika.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb)
kushoto akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Mhe. Nabil
Fahmy.
Mhe.
Membe na Mhe. Fahmy walifanya mazungumzo katika Hoteli aliyofikia
Waziri Membe. Mazungumzo yao yalihusu kuimarisha ushirikiano, Misri
kurejea katika Umoja wa Afrika na matumizi ya maji ya mto Nile.
Waziri
Membe akiwa na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wa Misri, Bi. Fatma.
Bi. Fatma ambaye alishawahi kufanya kazi katika Ubalozi wa Misri nchini
Tanzania ndio alikuwa Afisa Itifaki anayemuhudumia Mhe. Waziri na
ujumbe wake.
Waziri
Membe akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mawaziri wenzake baada ya
kushiriki katika chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa heshima yao na
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri
Waziri Membe (kushoto) akiongea
na Msaidizi wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri ambaye ana ngazi
ya Ukurugenzi kwenye chumba cha Wageni Maalum katika Uwanja wa Ndege wa
Cairo alipowasili kwa ajili ya kushiriki sherehe za kumuapisha Rais wa
nchi hiyo.
Waziri
wa Mambo ya Nje (kulia) akipokea taarifa fupi kutoka kwa Kaimu Balozi
wa Tanzania nchini Misri, Bw. Jestas Nyamanga katika Hoteli aliyofikia
Mhe. Waziri ya Fairmont.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb)
(kulia) akiwa katiika Kiwanja cha Ndege cha Addis Ababa akiwa njiani
kuelekea Cairo, Misri katika sherehe za kumuapisha Rais Mteule, Mhe.
Abdel Fattah al Sisi. Mwingine katika picha ni Bw, Shelukindo, Afisa wa
Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia.
Waziri Membe akibadilishana mawazo na watu mbalimbali kabla ya kupata Chakula cha Jioni.
Mhe.
Waziri Membe mwenye miwani akiwa amesimama mbele ya Hoteli ili kuingia
katika gari maalum kwa ajili ya kumpeleka eneo lililofanyika sherehe za
uapisho. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Afrika katika Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Vincent Kibwana.
Balozi
Kibwana (kushoto) akijadili jambo na Afisa wake, Bw. Celestine
Kakere.Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa