UCHAGUZI CHAMA CHA WANANCHI CUF WILAYA YA ARUSHA WAHIRISHWA MARA TATU
Mahmoud Ahmad Arusha
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/uchaguzi-chama-cha-wananchi-cuf-wilaya.html
Kutorudishwa
kwa majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali za chama wananchi(CUF)
wilayani Arusha kwa sababisha uchaguzi kuahirishwa mara tatu huku
mkutano mmoja ukishindwa kufikia Akidi kutokana na ibara ya
104 na 13 ya chama hicho.
Akizungumza
na mwanahabari msimamizi wa uchaguzi wa chama cha wananchi
(CUF)Mohammed Mtutuma alisema kuwa kutokana na ibara hiyo alilazimika
kuahirisha uchaguzi kama ibara hiyo inavysema kuwa kama haikufikia nusu
ya wajumbe basi uchaguzi hautafanyika.
Mtutuma
akatanabaisha kuwa kwa wilaya ya Arusha wajumbe waliohitajika kupiga
kura ni 180 na hadi wanaahirisha mkutano walikuwa wajumbe 53 hivyo
kutokana na akidi hiyo kama msimamizi aliahirisha uchaguzi huo kwani
wajumbe waliotakiwa walikuwa ni 91.
“Ni
kweli ndugu mwanahabari uchaguzi tumeahirisha kutokana na Akidi
kutotimia kwa kutofikia nusu ya koramu ya wajumbe walitakiwa kupiga kura
katika uchaguzi wa ngazi mbalimbali ndani ya chama wilayani Arusha na
utafanyika leo(jana) saa kumi jioni “alisema Mtutuma.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa mipago na uchaguzi wilayani hapa Omary
Salusingo alisema kuwa uchaguzi huo uliahirishwa kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo kutofikishwa kwa barua ya kutambulisha wagombea
kutoka makao makuu kwa ni siku ya kwanza tar.1 jun msimamizi aliwasomea
majina badala ya barua kutoka makao makuu.
Salusingo
alisema kuwa kutokana na hali hiyo ilibidi wakae kama kamati tendaji na
kuamuliwa uchaguzi kufanyika siku ya jumamosi tarehe 7 ambapo uchaguzi
huo uliahirishwa tena kutoka nakoramu ya wajumbe kutotimia na uchaguzi
kuamuliwa kufanyika siku nyingine itakayopangwa na uongozi wa wilaya.
Akilizungumzia
hilo katibu anayemaliza muda wake Zani Zakaria alisema kuwa suala hilo
la kuahirishwa kwa uchaguzi limesababishwa na makao makuu ya chama kwa
kutofuata kanuni za uchaguzi kwa kutoleta barua inayotambulisha wagombea
wa nafasi mbalimbali wanaotakiwa kugombea katika uchaguzi wetu.
Alisema
kuwa kutoka na hilo ndio kamati tendaji ikaamua kwenda kwenye uchaguzi
kwa shingo upande na majina waliosomewa na msimamizi wa uchaguzi
alietambuliwa kwa jina moja la Bobali hivyo kuonekana uchaguzi
unaendeshwa kinyume na kanuni za uchaguzi huku msimamizi huyo
akitusomea majina mawili kwa kila nafasi.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa CUF wilayani hapa Hamza Kidula alisema kuwa
yeye hana la kusema kwani kwa sasa ni mgombea hivyo aulizwe mkurugenzi
wa uchaguzi Omary Salusingo huku mkurugenzi wa mipango na uchaguzi taifa
Shaweji Mketo alisema kuwa kanuni ya uchaguzi ibara ya 13 ya CUF ndio
ilifuatwa.
Aidha
Mketo alisema kuwa utaratibu wa baraza kuu laCUF unatakiwa kupeleka
kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi majina matatu kwa kila nafasi huku
akimlaumu mwanahabari hii kwa kumuhukumu baada ya kmuuliza Swali kutaka
kufahamu juu ya uchaguzi huo ulioahirishwa mara tatu