TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/taarifa-ya-jeshi-la-polisi-mkoa-wa.html
MTU
MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA WOLTER JONATHAN (36) MKAZI WA MOROGORO
AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI NA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA.
AJALI HIYO
IMETOKEA MNAMO TAREHE 10.06.2014 MAJIRA YA SAA 04:30 JIONI KATIKA
BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE KATIKA KIJIJI CHA MBUYUNI, KATA YA
MAPOGORO, TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA
AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO,
JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALI YA SERIKALI MBARALI.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI
ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA
ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAFUNZI
WA DARASA LA KWANZA KATIKA SHULE YA MSINGI IDUDA ALIYETAMBULIKA KWA
JINA LA LEUS JOHN (07) MKAZI WA IDUDA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA
KUGONGWA NA GARI AINA YA TOYOTA COASTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA
DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
AJALI
HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 10.06.2014 MAJIRA YA SAA 20:40 USIKU KATIKA
BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU ENEO LA UYOLE – MAGOROFANI, KATA YA
IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI
MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI
ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA
ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
TAARIFA ZA MISAKO
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ASAJILE MWAKISAMBWE (41) MKAZI WA
KIJIJI CHA MAJENGO ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA
NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 52.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 10.06.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI KATIKA
KITONGOJI CHA MAJENGO, KIJIJI CHA UPENDO, KATA YA MAMBA, TARAFA YA
KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA
MTUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI
[GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WAPIGA
DEBE 09 WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA TUHUMA ZA
KUFANYA FUJO MAENEO YA STENDI YA MABASI ILOMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA
KUFUATI MGOMO WA DALADALA.
WATUHUMIWA
HAO NI PAMOJA NA 1. IPYANA MWANGOMOLE (27) MKAZI WA MAKUNGULU 2.
HUSSEIN HASSAN (32) MKAZI WA ILEMI 3. ZAKARIA LIANDA (23) MKAZI WA
AIRPORT 4. BAHATI MATHIAS (28) MKAZI WA SAE 5. BONIFACE JASSON (22)
MKAZI WA ITUHA 6. AMOS ROBERT (16) MKAZI WA SAE 7. OTTO JEKI (21) MKAZI
WA ILOMBA 8. ALEX MWAIKUJI (28) MKAZI WA AIRPORT NA 9. LEOFASI ANTHONY
(17) MKAZI WA SAE. WATUHUMIWA WALIKUWA WAKIWA WANAFANYA FUJO KUFUATIA
MGOMO WA DALADALA.
WATUHUMIWA
HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 10.06.2014 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA
KATIKA STENDI YA MABASI ILOMBA, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI
NA MKOA WA MBEYA.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA KUFANYWA.
Imetolewa na:
[BARAKAEL MASAKI – ACP]
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.