Sketi fupi; Polisi akwenda mahakamani
Koplo wa polisi matatani eti sketi imembana
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/sketi-fupi-polisi-akwenda-mahakamani.html
Koplo wa Kitengo cha Traffiki
aliyepigwa picha akiwa amevalia sketi iliyomabana makalio amelazimika
kukimbilia mahakamani kuokoa kazi yake.
Linda Okello alikimbilia Mahakamani Baada ya
wakubwa wake kutaka kumchukulia hatua ya kinidhamu wakidai alikosa
nidhamu ya kazi alipovalia sketi iliyoonesha umbo lake akiwa kaziniDada huyo aliyezua mjadala kote duniani kuhusu wanawake waliojaliwa makalio makubwa na kama wanabaguliwa kutokana na maumbile yao amemshtaki Inspekta mkuu wa polisi nchini Kenya miongoni mwa tume inayosimamia polisi nchini humo.
Koplo Linda anasema kuwa Afisa mkuu wa wilaya ya kiambu Stephen Ngetich hata hakuwepo katika eneo la tukio lakini ndiye aliyemshmtaki.
Linda alipigwa picha akilinda usalama katika mashindano ya mbio za magari ya Kiambu na picha hiyo ikaenea sana katika mitandao ya kijamii kuhusiano na urefu wake na pia makalio na umbo lake .
Aidha koplo huyo huyo anasema kuwa japo alipewa Suruali ndefu mbili iliasiivae tena sketi hiyo yake ,Koplo anadai kuwa bosi wake hakuwahi kumkaripia kwa kuivalia na kuwa madai dhidi yake yanashinikizwa tu na watu waliovutiwa na mjadala katika mitandao ya kijamii.
Alipigwa picha na mwanahabari mmoja wa gazeti moja maarufu nchini Kenya akiwa na wenzake kazini mjini Kiambu.
Lakini punde si punde picha hiyo ikaanza kusambazwa kwa mitandano ya kijamii na baadhi wakiikejeli.
Taarifa ya polisi huyo kuonywa ilizua hasira kwenye mitandao ya kijamii baadhi wakihoji ikiwa ni makosa kwa afisaa wa polisi kuvalia sketi ya kumbana.
Nini Kauli yako?