RIBERY ANAWEZA KUKOSA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA, LAKINI HAIFUNGUI MLANGO KWA SAMIR NASRI
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/ribery-anaweza-kukosa-fainali-za-kombe.html
Coach Didier Deschampnyota alisema atafanya kila linalowezekana kumsaidia nyota wake acheze fainali za kombe la dunia.
Imechapishwa Juni 4, 2014, saa 10:01 jioni
WINGA
wa Bayern Munich, Frank
Ribery bado yuko kwenye hofu kubwa ya kutoiwakilisha Ufaransa katika
fainali za kombe la dunia nchini Brazil, lakini Samir Nasri hataitwa
kama mbadala wake.
Jumatatu
ya wiki hii, Ribery alitajwa katika kikosi cha wachezaji 23 tayari kwa
safari ya Brazil , lakini bado yuko katika wasiwasi kama ataimarika
majeruhi yake ya mgongo.
Remy
Cabella wa Montpellier - ambaye anawindwa na Newcastle - na mchezaji
wa Lyon, Alexandre Lacazette wako makini kusikilizia nafasi hiyo endapo
Ribery atashindwa kupona.
Nyota huyo mwenye miaka 31 alikosekana
katika ushindi wa mabao 4-0 ambao Ufaransa ilipata jumanne katika mechi
ya kirafiki dhidi ya Norway.
Pia alitokea benchi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Paraguay ambapo timu hizo zilitoka sare ya 1-1.
Shirikisho la soka nchini Ufaransa
liliripotiwa likisema kuwa ijumaa ya wiki hii ndio siku ya mwisho
kusubiri kama Ribery ataimarika, lakini inaonekana limeamua kumuacha
mpaka atakapokuwa tayari.
Kinadharia, Deschamps atasubiri mpaka
zibaki saa 24 kucheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Honduras juni 15 ili
kutangaza mbadala wa Ribery.