Rais Rouhani wa Iran ziarani nchini Uturuki
Rais Hassan Rouhani wa Iran
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/rais-rouhani-wa-iran-ziarani-nchini.html
Rais Hassan Rouhani wa Iran
Rais
Hassan Rouhani aliyefuatana na ujumbe mkubwa wa serikali yake amepangiwa
kukutana na maafisa wa serikali ya Uturuki,ikiwa ni pamoja na rais
Abdullah Gul na waziri mkuu Recep Tayyeb Erdogan mjini Ankara.Mada
mazungumzoni zitahusu usalama pamoja pia na biashara kati yao.Iran na
Uturuki zimepangiwa kusimamia kwa pamoja kikao cha kwanza cha baraza la
ushirikiano-taasisi iliyoanzishwa na Ankara kwa lengo la kuhimiza
biashara ya kimkoa.(Martha Magessa)
Kabla ya
kuondoka Teheran,rais Rouhani alinukuliwa na shirika la habari la
Iran-Irna akisema atalizusha pia suala la Syria pamoja pia na lile la
Irak wakati wa mazungumzo yake pamoja na viongozi wa mjini Ankara.
Hali ya mambo katika eneo la Afrika kaskazini,Palastina na mashariki ya Kati nayo pia itajadiliwa.
"Ni
muhimu kuzungumzia masuala yote hayo pamoja na Uturuki" rais Rouhani
amenukuliwa na shirika rasmi la habari la Iran-Irna akisema na
kusisitiza "kuimarishwa uhusiano wa pande mbili "ni muhimu kwa eneo lote
hilo."
Biashara ya pande mbili itaimarishwa
Waziri mkuu Erdogan alipoitembelea Iran mwishoni mwa mwezi wa januari mwaka huu
Ziara ya
rais Rouhani mjini Ankara inatokea muda mfupi tu tu kabla ya mazungumzo
ya ana kwa ana ya mjini Gevena kati ya Iran,Marekani,na Umoja wa ulaya
kuhusu mradi wa nuklea wa Iran.
Rais
Rouhani anatarajiwa kutia saini makubaliano yatakayoimarisha uhusiano
pamoja na Uturuki-uhusiano uliodhoofika kutokana na vita nchini Syria
ambako serikali ya Iran inaiunga mkono serikali ya ya rais Bashar al
Assad huku Uturuki ikiwaunga mkono waasi.
Makubaliano ya kiuchumi na hasa ushirikiano katika sekta ya nishati,gesi na umeme yanatarajiwa kutiwa saini.
Waziri
mkuu wa Uturuki Recep Tayyeb Erdogan alifika ziarani nchini Iran januari
mwaka huu.Wakati ule alizungumzia azma ya kuzidisha kiwango cha
biashara ya pamoja kati ya nchi zao mbili toka dala bilioni 13.5 mwaka
2013 na kufikia dala bilioni 30 ifikapo mwaka 2015.
Ikitegemea
kwa sehemu kubwa nishati kutoka Iran na Urusi,Uturuki inapanga
kuzidisha kiwango cha mafuta na gesi kuoka Iran pindi vikwazo vya
kimataifa vikiondolewa,makubaliano yatakapofikiwa kuhusu mradi wa
kinuklea wa Iran mjini Geneva.
CHANZO:DW