MAMA SALMA KIKWETE MGENI RASMI KWENYE TAMASHA LA KWANZA LA VITABU VYA HADITHI KWA WATOTO WA SHULE ZA MSINGI
https://samchardtz.blogspot.com/2014/06/mama-salma-kikwete-mgeni-rasmi-kwenye.html
Baadhi
ya watoto wa shule za msingi jijini Dar wakifanya mazoezi ya maigizo
kwa ajili ya tamasha la kesho kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
WANAFUNZI
wa shule za Msingi nchini, wameshauriwa kuwa na mazoea ya kusoma vitabu
kwa lengo la kuwa wagunduzi wa vitu mbalimbali.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Soma, Demere
Kitunga wakati wa maandalizi ya tamasha la kwanza la vitabu vya hadithi
kwa watoto wa Shule za msingi.
Kitunga
amesema kuwa tamasha hilo ni moja ya michakato ya kuwataka watoto
kupenda kusoma vitabu hasa vitabu vya hadithi kwa nia ya kujifunza mambo
mbalimbali ya kijamii.
"Ugunduzi
wa jambo fulani unaanzia katika kusoma hivyo watoto wakiwa wanania ya
kusoma vitabu mbalimbali hususani vya hadithi wataweza kuongeza uwelewa
fulani katika fikra zao,"amesema Kitunga
Aidha
amesema kuwa tamasha hilo linatarajia kuanza kesho hadi juni 14 mwaka
huu katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini ,ambapo Mgeni rasmi
anatarajia kuwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Mmoja
wa watoto akionyesha kipaji chake wakati wa mazoezi kwa vitendo kupitia
hadithi mbalimbali walizosoma kutoka kwenye vitabu.
Kitunga
amesema kuwa Taasisi hiyo hadi sasa imeweza kusambaza vitabu katika
Shule mbalimbali za Msingi pamoja na klabu za kujisomea zikiwemo
Kurasini ,maktaba pamoja na Chang'ombe.
Alisema
katika tamasha hilo kutakuwa na maigizo ambayo yatafanywa kwa kutumia
hadithi zilizokuwa katika vitabu hii yote kwa lengo la kukuza utamaduni
wa watoto kusoma vitabu.