Flatnews

GRAND MALT YADHAMINI TAMASHA LA FILAMU MTWARA


Meneja masoko wa Tbl Fimbo Buttala katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kuzunduliwa kwa tamasha kubwa la Filamu litakalofanyika mkoani Mtwara ambapo litashirikisha jumla ya wasanii arobaini nchini,kulia ni mratibu wa tamasha hilo Musa Kisoki na mwakilishi wa Bongo Muvie Shashim kambi 
KAMPUNI ya Bia Nchini (TBL) kupitia kinywaji chake cha Grand Malt kimetangaza kudhamini tamasha la wazi la  filamu ‘Tanzania Open Festival’ litakalofanyika mapema mwezi Agosti mwaka huu mkoani Mtwara. Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kwa muda wa wiki moja kuanzia sikukuu ya Eid Pili hadi Agosti 5 mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana , Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah, alisema kuwa tamasha la mwaka huu  litafanyika mkoani Mtwara kwenye viwanja vya Mashujaa na hii imetokana na muonekano mkubwa uliopatikana mwaka jana.

Butallah alisema kuwa  lengo la kudhamini tamasha hili ni kutoka nafasi kwa mashabiki wa sanaa ya filamu nchini kushuhudia kazi zilizoandaliwa na wasanii wa hapa nchini. Butallah alisema kuwa wanaamini kufanyika kwa tamasha hili kunasaidia kukuza filamu za wasanii hao ambao wanapata ajira kupitia kazi wanazozifanya ambazo pia huburudisha jamii. Alisema tamasha hili linasaidia kutoa nafasi kwa wasanii wa Tanzania kubadilishana mawazo na wadau ambao wananunua kazi zao.

“Tamasha hili tunaamini litatoa nafasi na kwa wapenzi wa Bongo Movie wa mkoa wa Mtwara na jirani kuona filamu zetu za kitanzania,” alisema Butallah. Alisema kwamba kwa kushirikiana na kampuni ya Sophia Records , TBL itahakikisha filamu za wasanii wa Kitanzania zinajulikana na kupata soko ndani na nje ya nchi.

Mratibu wa tamasha hilo, Mussa Kisocky, wanawashukuru wadhamini kwa sababu wamesaidia kulikuza na kufikisha ujumbe wa walengwa. Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ni Amani na Upendo na wakiwa huko wasanii wanapata nafasi ya kutembelea shughuli mbalimbali za kijamii.

Alieleza kwamba mwaka huu wanatarajia kutoa vyandarua na magodoro kwa ajili ya wodi ya wanawake na watoto ya hospitali ya mkoa huo. “Ni chombo kinachowakusanya wasanii na wananchi wanaoona kazi zao,” alisema Kisocky. 

Mwakilishi kutoka Bongo Movie, Athumani Kambi, mbali na kupata nafasi ya kukutana na mashabiki wao, pia hukutana na wasanii chipukizi na kuwaelekeza njia sahihi ya kujiendeleza na kukuza vipaji vyao. Grand Malt inadhamini tamasha hili kwa mara ya tatu mfululizo ambapo mwaka juzi lilifanyika jijini Tanga na mwaka jana lilikuwa Mwanza.

Post a Comment

emo-but-icon

item