Flatnews

USIOMBE UKAPATWA NA GONJWA HILI, NDUGU NA WATOTOT WAMTENGA MAMA HUYU

MARY Izengo (52), mkazi wa Kijiji cha Umanda- Msalala, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza anateseka kiasi cha kutamani afe kufuatia gonjwa...



MARY Izengo (52), mkazi wa Kijiji cha Umanda- Msalala, Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza anateseka kiasi cha kutamani afe kufuatia gonjwa la ajabu alilonalo huku akisema ndugu, wakiwemo watoto wake wamemtenga.
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Wadi Namba 23, Jengo la Sewa Haji kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, mwanamke huyo alisema usiombe gonjwa hilo liliompata akiwa na umri wa miaka 5 likupate kwani ugonjwa unaomkabili ni wa uvimbe mkubwa usoni ambapo unamtesa kwa kipindi kirefu huku akionekana  kero kubwa katika jamii.
Mary aliendelea kusema kuwa, siku moja alijikuta akisukumwa kwenda kwenye mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Nyang’wale wilayani Geita, Mhe. Ahmed Nassor Amar ‘Gulamali’.

 Haikuwa kawaida yangu kushiriki mikutano, lakini siku hiyo nilikwenda. Mwisho wa mkutano, mbunge aliniona akanihurumia sana na kuniambia nije Muhimbili nipatiwe matibabu, akanipa shilingi laki tatu.
Ndipo Aprili mwaka huu nikamtafuta msamaria mwema, akanileta hapa Muhimbili ambapo madaktari wamenipokea vizuri sana

Madaktari walinifanyia uchunguzi na wakanieleza kwamba kuna mshipa unapitisha damu kwa wingi ndiyo maana nimevimba hivi, wakasema matibabu yake hapa nchini haiwezekani mpaka India. Kwa hiyo kwa sasa nasubiri kama nitaweza kwenda huko.
 Kinachonishangaza na kunisikitisha ni kwamba, hapa Dar es Salaam nina kaka yangu, nilipofika tu hapa hospitali nilimuomba muuguzi simu nikampigia kumjulisha kuwa naumwa nipo Muhimbili. Miaka mingi hatujaonana akafikiri kuwa ugonjwa wangu ni wa kawaida. 
Alipokuja na kuniona alitokwa machozi na kuondoka. Kuanzia hapo kila nikimpigia simu hapokei
alisema mama huyo.
Mary anaomba msaada ili aweze kupata fedha zitakazomuwezesha kwenda India kutibiwa. Ukitaka kumsaidia tuma fedha kwa namba 0683 406 680 ya afisa ustawi wa jamii aliye karibu naye.

Post a Comment

emo-but-icon

item