MAPACHA WAZALIWA WAKISHIKANA MIKONO
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/mapacha-wazaliwa-wakishikana-mikono.html
Mama mmoja nchini Marekani, amejifungua mapacha waliozaliwa wakiwa wameshikana mikono.
Watoto hao pia walikuwa wanapumua bila usaidizi wowote walipotolewa kutoka katika mashine yenye hewa ya Oxygen.
Mama wa watoto hao, alisema kuwa watoto hao waliopewa majina ya
Jillian na Jenna Thistlewaite walikuwa wameshikana katika kitovu na
kutumia Kondo la nyuma moja , hali ambayo madaktari walisema ni ya
kipekee.
"Tayari ni marafiki ,’’ alisema mama yao Sarah Thistlethwaite.
Walizaliwa Ijumaa katika jimbo la Ohio, wakiwa wameshikana mikono.
Inaarifiwa ni mama mmoja tu kati ya akina mama elfu kumi mwenye uwezo wa kujifungua mapacha wa aina hiyo.
Bi Thistlewaite, mwenye umri wa miaka 32,alilazimika kupumzika kwa
wiki kadhaa kabla ya kujifungua kwani mapacha wanaozaliwa wakiwa
wameshikana mikoni ni hali nadra ambayo inaweza kuhatarisha maisha ya
watoto hao kabla ya kuzaliwa.
Mama huyo alisema kupokea watoto wake ilikuwa zawadi tosha kwake
wakati huu wa kusherehekea siku ya akina mama duniani.Chanzo BBC Swahili