CHEKI MATAJIRI WA MAN CITY WALIVYOSHEREHEKEA UBINGWA WA LIGI KUU ENGLAND
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/cheki-matajiri-wa-man-city.html
Wanakata kepi yao ya ubingwa: Sheikh Mohammed akisherehekea ubingwa wa Man City kiaina yake.
WAKATI
wachezaji wa Manchester City walishereheka kwa mbwembwe taji la ubingwa
wa Ligi Kuu ya England, wamiliki wa timu hiyo walifanya sherehe ndogo
tulivu kufurahia ubingwa wa pili wa ligi hiyo ndani ya misimu mitatu.
Wachezaji
waliangusha pati Uwanja wa Etihad na baadaye waakenda kujirusha Town
Hall na nyota wa Oasis, Noel na Liam Gallagher na miga gita wa Smiths,
Johnny Marr.
Lakini
Sheikh Mansour alisherehekea ubingwa huo wa City kwa kukata keki maalum
iliyotengenezwa kitaalamu katika muundo wa Uwanja na taji hilo la
ubingwa wa Ligi Kuu.