KINDA LA MAN UNITED, ADNAN YUNAZAJ LAITWA TIMU YA TAIFA YA UBELGIJI, MAJEMBE YOTE YA KAZI HAYA HAPA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/kinda-la-man-united-adnan-yunazaj.html
KOCHA
wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Marc Wilmots ametaja kikosi chake kwa ajili ya
kombe la dunia na kumujumuisha kinda wa Manchester United Adnan Junazaj.
Ubelgiji
imepangwa kundi H na timu za Russia, Algeria na kurea kusini ambao wataanza
kampeni zao juni 17 dhidi ya Algeria.
Wilmots
ametangaza kikosi cha wachezaji 24 na wengine 6 wa ziada kama itatokea majeruhi
katika kikosi chake.
Mbali
na kinda huyo mwenye miaka 19 , Thibaut Courtois, Jan Vertonghen, Vincent
Kompany Dries Mertens, Eden Hazard, Marouane Feillaini na Romelu Lukaku, Axel Witsel wamejumuishwa
katika kikosi hicho.
Ajabu
nyingine ni kujumuishwa kwa mshambiliaji wa Lille ya ufaransa mwenye miaka 19, Divock Origi, ambaye amefunga mabao matano
katika mechi 29 alizocheza Ligue 1 msimu
huu.
Kikosi
kizima hiki hapa:
Walinda Mlango: Thibaut
Courtois, Simon Mignolet, Koen Casteels, Silvio Proto
Mabeki: Toby
Alderweireld, Laurent Ciman, Anthony Vanden Borre, Vincent Kompany, Daniel Van
Buyten, Jan Vertonghen, Thomas Vermaelen, Nicolas Lombaerts
Viungo: Axel Witsel,
Steven Defour, Marouane Fellaini, Mousa Dembele, Nacer Chadli, Kevin De Bruyne
Washambuliaji: Eden Hazard,
Romelu Lukaku, Divock Origi, Dries Mertens, Kevin Mirallas, Adnan Januzaj
Wachezaji wa akiba: Sebastien
Pocognoli, Jelle Van Damme, Thorgan Hazard, Radja Nainggolan, Michy
Batshuayi, Guillaume Gillet