SIMBA WASIOFUGIKA CAMEROON WATAJA KIKOSI CHA AWALI CHA WACHEZAJI 28 KOMBE LA DUNIA....SAMUEL ETO`O NDANI
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/simba-wasiofugika-cameroon-wataja.html
SAMUEL Eto`o ametajwa katika kikosi cha awali cha
wachezaji 28 cha timu ya taifa ya Cameroon kwa ajili ya fainali za kombe la
dunia mwezi ujao nchini Brazil.
Kocha Volker Finke amemuita Eto`o na kumfanya
nyota huyo wa Chelsea acheze fainali zake za nne za kombe la dunia.
Eto`o alicheza
fainali za kwanza za kombe la dunia mwaka 1998, akaja kucheza 2002 na 2010
nchini Afrika kusini, na kama atacheza fainali za mwaka huu basi nyota huyo
mwenye miaka 33 atafikia rekodi ya Rigobert
Song na Jacques Songo, ambao waliichezea
Cameroon katika fainali nne za kombe la dunia.
Eto`o ambaye alitangaza kustaafu soka la
kimataifa mwaka jana, lakini akabadilisha maamuzi yake pia anatarajia kufikia
rekodi ya mabao ya Roger Milla.
Nyota huyo wa zamani
wa Cameroon alifunga mabao 5 katika fainali zote za kombe la dunia alizoichezea
nchi yake, lakini Eto`o amefunga mabao mawili tu katika fainali tatu alizocheza.
Cameroon
wataanza kampeni za kombe la dunia kwa kuvaana na Mexico juni 14 kabla ya
kukutana na Croatia na wenyeji Brazil waliopo kundi A.
Kikosi
cha awali cha wachezaji 28 cha timu ya
taifa ya Cameroon kwa ajili ya kombe la dunia hiki hapa;
Walinda
mlango:
Loic Feudjou (Coton Sport), Charles Itandje (Konyaspor), Sammy N'Djock
(Fethiyespor), Guy N'dy Assembe (Guingamp).
Walinzi:
Benoit Assou-Ekotto (QPR), Henri Bedimo (Lyon), Gaetan Bong (Olympiacos),
Aurelien Chedjou (Galatasaray), Cedric Djeugou (Coton Sport), Jean-Armel
Kana-Biyik (Rennes), Nicolas N'Koulou (Marseille), Dany Nounkeu (Besiktas),
Allan Nyom (Granada).
Viungo:
Eyong Enoh (Antalyaspor), Raoul Loe (Osasuna), Jean Makoun (Rennes), Joel Matip
(Schalke), Stephane Mbia (Sevila), Landry N'Guemo (Bordeaux), Edgar Salli
(Lens), Alex Song (Barcelona).
Washambuliaji:
Vincent Aboubakar (Lorient), Maxim Choupo-Moting (Mainz), Samuel Eto'o
(Chelsea), Mohammadou Idrissou (Kaiserslautern), Benjamin Moukandjo Nancy),
Fabrice Olinga (Zulte Waregem), Pierre Webo (Fenerbahce).
On
standby: Frank Bagnack (Barcelona), Zock Bep (Cosmos de Bafia).