RIO FERDINAND `BAI BAI` MANCHESTER UNITED, ANYIMWA MKATABA MPYA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/rio-ferdinand-bai-bai-manchester-united.html
MAISHA ya Rio
Ferdinand katika klabu ya Manchester United yamefikia kikomo baada ya mkongwe huyo kupewa taarifa kuwa hataongezewa mkataba.
Inafahamika
kuwa mkurugenzi mkuu wa Old Trafford, Ed Woodward alimwaga mchele kwa
Ferdinand mwenye miaka 35 kwenye chumba cha kubadilishia nguo siku ya
jumapili katika mchezo wa sare 1-1 dhidi ya Southampton.
Watu
wengi walikuwepo katika chumba hicho na kushangazwa na taarifa ya
Woodward ambaye aliweka mamboo hadharani kuwa miaka 12 ya Ferdinand
inatosha kabisa na ataondoka majira ya kiangazi mwaka huu.
Beki
huyo wa zamani wa England aliwaambiwa wachezaji wenzake kuwa sare ya
1-1 katika dimba la St Mary ndio mchezo wake wa mwisho na aliomba
kusaini mpira ili kuacha kumbukumbu yake.
Rio Ferdinand ataondoka Manchester United kama mchezaji huru baada ya klabu yake kusema haitamuongezea mkataba
Ferdinand aliyedumu Man United kwa
miaka 12, alipigwa picha akichuana na Frank Ribery wa Bayern Munich
kwenye mechi ya robo fainali ya UEFA
Historia nzuri: Ferdinand alibeba kombe
la UEFA mwaka 2008 akiwa na mkongwe mwenzake, Ryan Giggs baada ya
kuifumua Chelsea kwa penati.
Benchi sana: Ferdinand alihangaika sana kupata nafasi ya kucheza wakati wa utawala wa David Moyes mapema msimu huu
Mtu shujaa: Ferdinand alisindikizwa
kutoka nje ya uwanja na Robin van Persie baada ya kurushiwa shilingi na
kuumizwa katika mchezo wa watani wa jadi wa jiji la Manchester mwaka
2012.