MWANAMKE MIAKA 70 AUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/mwanamke-miaka-70-auawa-na-watu.html
“PRESS RELEASE”TAREHE 06.05.2014.
- MWANAMKE WA MIAKA 70 AUAWA NAWATU WASIOFAHAMIKA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA SHAMBANI.
- MZEE WA MIAKA 70 AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI RUNG
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA MBALIMBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MWANAMKE
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MESIA SHOTI (71) MKAZI WA KIJIJI CHA
SISITILA ALIKUTWA AMEBAKWA KISHA KUUAWA KWA KUPIGWA NA VITU BUTU
SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA NA KISHA MWILI WAKE
KUTUPWA SHAMBANI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 05.05.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA SISITILA, KATA YA SISITILA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA
MKOA WA MBEYA. MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA NA JERAHA SEHEMU ZA KICHWANI.
CHANZO CHA TUKIO HILO BADO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA MBEYA.UCHUNGUZI ZAIDI WA TUKIO HILI
BADO UNAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA
NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MZEE
WA MIAKA 70 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MKISU LEMBUKA MKAZI WA KAYUKI
AMEFARIKI DUNIA WAKATI ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA SERIKALI
MAKANDANA –TUKUYU WILAYA YA RUNGWE BAADA YA KUGONGWA NA GARI
LISILOFAHAMIKA.
AWALI
MNAMO TAREHE 04.05.2014 MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI
CHA KAYUKI, KATA NA TARAFA YA TUKUYU GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA
LILIMGONGA MZEE HUYO NA KUMSABABISHIA MAJERAHA. CHANZO CHA AJALI NI
MWENDO KASI. DEREVA AMBAYE PIA HAKUFAHAMIKA ALIKIMBIA NA GARI MARA
BAADA YA TUKIO.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA
MIGUU KUTEMBEA PEMBENI MWA BARABARA NA KUVUKA SEHEMU ZENYE VIVUKO ILI
KUEPUKA AJALI .AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA MISAKO:
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA NEFA LETSON (30) MFANYABIASHARA, MKAZI WA LUPA-DARAJANI AKIWA NA
POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA RIDDER
KATONI 12 NA BOSS KATONI 01.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 05.05.2014 MAJIRA YA
SAA 15:30 ALASIRI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA LUPA –DARAJANI, KIJIJI CHA
KIBAONI, KATA YA CHOKAA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA
MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBEHIZO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI MTUHUMIWA ZINAFANYIKA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUACHA KUUZA/KUSAMBAZA BIDHAA
ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
KATIKA
MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA
RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MHAMIAJI
HARAMU ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA KATIKA ENEO LA ITEZI, KATA
YA ITEZI, TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA
KUMKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAFANYIKA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU
WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO ILI WAKAMATWE NA UCHUNGUZI DHIDI
YAO UFANYIKE.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.