MAAJABU: MBWA ADAIWA KUZAA SUNGURA, PICHA NA TUKIO HUSIKA LIPO HAPA
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/maajabu-mbwa-adaiwa-kuzaa-sungura-picha.html
WENYEJI
wa kijiji cha Kithenge kutoka wilaya ya Igembe kusini wamebaki vinywa
wazi kufuatia tukio la kustaajabisha ambapo mbwa wa jirani yao
alijifungua sungura badala ya mbwa wa kawaida.
Kulingana
na mwnenye mbwa huyo Bw Josphat Kairithia, kitendo hiki kilitokea
Jumanne wiki iliyopita ambapo alimpata mbwa huyo akimyonyesha na
akadhania ni mbwa wa kawaida.
Baada
ya kuchunguza zaidi, aligundua kuwa hakuwa mbwa wa kawaida bali sungura
na hapo ndipo alianza kuwaita majirani wake waje kumtegulia kitendawili
hicho.
Hata hivyo, waliokuja walishtuka zaidi na wengine wakitoroka wakidhania kuwa hayo yalikuwa mazingaombwe.
“Tukio
hili limenishangaza sana na siwezi nikaeleza kilichotendeka.
Anamnyonyesha sungura huyu kama kawaida na hataki kumuona mtu
akimkaribia. wanaokuja kumwona lazima wapitie kwangu ili niweze
kumtuliza mbwa huyo la sivyo wakipate cha mtema kuni,” akasema.
Kairithia
alitupilia mbali uwezekano kuwa hayo yangekuwa mazingaombwe huku
akielezea kuwa huenda ikawa ni ujumbe kutoka kwa mungu kuwaambia watu
wapende maadui wao.
“Siwezi
nikasema kuwa haya ni mazingaombwe kwani najua ya kwamba mungu ana njia
nyingi za kuongea na watu wake. Labda anataka kutuelezea jinsi ambavyo
tunapaswa kuwapenda hata wale ambao tunafikiri ni maadui wetu,” akasema.
Sungura mwingine
Ametupilia
mbali fununu za watu ambao wanadai kuwa huenda alimwekea mbwa huyo
sungura huyo akisema kuwa hakuwa karibu mambo hayo yakitendeka.
Ili
kutoa thibitisho kwa watu, Kairithia alimwekelea sungura mwingine
karibu na mbwa huyo na kilichowashangaza wengi ni kuwa hakupoteza muda
kumla.