LE MAJANGAZ MUME ADAIWA KUUZA KABURI LA MKE WAKE
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/le-majangaz-mume-adaiwa-kuuza-kaburi-la.html
Shakoor Jongo na Deogratius Mongela
Mwanaume
aliyetajwa kwa jina moja la Abrahaman, mkazi wa Kimara-Kilungule, Dar,
anadaiwa kuuza kiwanja ambacho ndani yake kuna kaburi marehemu mkewe,
Aisha Abdul aliyefariki Julai 21, 2004.
MALALAMIKO MEZANI
Wakizungumza
na Uwazi kwa nyakati tofauti, watoto wa marehemu ambao wanapingana na
tukio hilo la baba yao kuuza eneo hilo ambalo ni mali ya marehemu mama
yao, walidai kuwa wamefedheshwa na kitendo hicho.
“Kiukweli
alichokifanya baba siyo sawa. Haiwezekani auze eneo ambalo lipo kaburi
la mama yetu. Mbaya zaidi hadi sisi watoto wa kutuzaa yeye mwenyewe
anatutishia maisha.
“Anatufukuza
katika nyumba kisa kwa nini tunamuhoji tabia yake ya kuuza maeneo
aliyoyaacha marehemu mama,” alisema Tunu ambaye ndiyo msimamizi mkuu wa
mirathi.
Watoto hao
walidai kuwa baba yao anauza mali huku akijua kabisa mama yao aliacha
wosia juu ya nani mrithi wa mali hizo (kopi ya wosia tunayo).
“Hatujui
nini kimemkumba baba maana amekuwa mkatili asiyekuwa na huruma ya aina
yoyote kwetu hadi na kwa majirani,” walisema watoto hao.
USHUHUDA
Gazeti
hili lilifika eneo la tukio na kulishuhudia kaburi hilo huku watoto hao
wakipiga nalo picha kwa woga wasikute na aliyeuziwa.
Pia majirani walithibisha ukali wa baba huyo katika siku za hivi karibuni.
Katika
hali ya kushangaza, wakati watoto hao wakitoa malalamiko hayo walianza
kugawanyika kifamilia ambapo mmoja wa mwisho wa kiume alikuwa upande wa
baba akiunga mkoni kile alichokifanya mzazi wake huyo.
Baada ya kusikia malalamiko hayo na kuoneshwa vielelezo, ilibidi kumtafuta mume huyo wa marehemu ili kuthibitisha madai hayo.
Alipopatikana
alipelekewa tuhuma zake juu ya sakata ambapo bila hata kusikia kwa
makini alichokuwa akielezwa alianza kutukana huku akilichimba mkwara
Uwazi kufuatilia habari zake.
“Endeleeni kunifuatilia lakini mtakachokiona nisilaumiwe,” alisema baba huyo aliyeonekana kuwa na umri mkubwa.
Katika hitimisho, watoto hao walishauriwa kwenda kwenye vyombo au mamlaka za kisheria ili kupata haki zao.