KIMENUKA TOTTENHAM HOTSPURS, TIM SHERWOOD KITUMBUA CHAINGIA MCHANGA, AFUTWA KAZI
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/kimenuka-tottenham-hotspurs-tim.html
Amesepa: Tim Sherwood amefukuzwa kazi katika nafasi yake ya ukocha mkuu Tottenha.
TIM Sherwood amefukuzwa kazi Tottenham Hotspur kama kocha mkuu baada ya kudumu kwa miezi sita tu kwenye uwanja wa White Hart Lane.
TIM Sherwood amefukuzwa kazi Tottenham Hotspur kama kocha mkuu baada ya kudumu kwa miezi sita tu kwenye uwanja wa White Hart Lane.
Sherwood
alirithi
mikoba ya Andre Villas-Boas mwezi desemba mwaka jana kwa mkataba wa
miezi 18, lakini ameshindwa kufikia msimu wake wa pili baada ya kibarua
chake kuota nyasi.
Sherwood
alishinda mechi14 katika michezo 28 aliyoiongoza Spurs na kumaliza nafasi ya 6 katika msimamo.
Hata hivyo, kocha huyu mwenye miaka 45
anaweza kupewa ofa nyingine ya kazi katika klabu inayocheza
Championship ya Brighton baada ya aliyekuwa kocha wake Oscar Garcia
kujiuzulu kufuatia kufungwa na Derby.
Levy amesema katika mtandao wa klabu: 'Tulimteua Tim katikati ya msimu kwasababu alikuwa anawajua wachezaji wa klabu.
"Tulikubaliana mkataba wa miezi 18 lakini tulizungumza kuvunja mkataba mwishoni mwa msimu na tumefanya hivyo".
"Kwa niaba ya klabu, tunamshukuru kwa jitihada zake kwa miaka aliyokaa
nasi. Tunamtakia mafanikio makubwa katika kazi yake ya ukocha'".