KAULI YA KIKWETE KUHUSU DENGUE
https://samchardtz.blogspot.com/2014/05/kauli-ya-kikwete-kuhusu-dengue.html
Wakati
raia tisa wa China wakibainika kuugua ugonjwa wa dengue na kulazwa hapa
nchini, Rais Jakaya Kikwete amevunja ukimya na kuagiza wizara zake
mbili kukabiliana na ugonjwa huo kwa dharura.
Ugonjwa
huo uliingia nchini tangu mwaka 2010 lakini mlipuko wake mkubwa
ulibainika Machi mwaka huu na hadi jana wagonjwa zaidi ya 400 walikuwa
wameambukizwa, huku watatu wakiripotiwa kufariki dunia, akiwamo Daktari
Bingwa wa magonjwa ya akili, Dk Gilbert Buberwa anayezikwa leo, Dar es
Salaam.
Rais
jana aliziagiza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na ile ya Fedha
kushirikiana Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuchukua hatua za dharura
kupambana nao kwa kuhakikisha vinapatikana vipimo vya kutosha na dawa.